MISA-TAN YAWATUNUKU TUZO ZA HESHIMA WAJUMBE WA BODI ILIYOMALIZA MUDA WAKE


Mwenyekiti wa MISA-TAN Salome Kitomari aliyemaliza muda wake akipewa Tuzo ya heshima.

Na Marco Maduhu,DODOMA

TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini Mwaka Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) imewatunuku Tuzo za heshima wajumbe wa bodi wa taasisi hiyo ambao wamemaliza muda wao.

Tuzo hizo zimetolewa leo Machi 14,2025 kwenye Mkutano wa MISA-TAN na wadau wa habari Jijini Dodoma.

Bodi ya MISA-TAN iliyopita ilifanya kazi zake ndani ya miaka 8, mpaka hapo uchaguzi wa viongozi wapya uliofanyika Desemba 4 mwaka 2024,na kumchagua Edwin Soko kuwa Mwenyekiti mpya wa MISA-TAN.
Wajumbe hao wa Bodi waliomaliza muda wao ni Salome Kitomari ambaye alikuwa Mwenyekiti, James Malenga Makamu Mwenyekiti,wakifuatiwa na wajumbe wengine ni Mussa Juma, Michael Gwimila na Idda Mushi.

Aidha, katika mkutano huo pia MISA-TAN iliwatunuku vyeti vya pongeza wadau ambao ni PSSSF,NSSF,TCRA,PCCB,TASAF,TASHICO,NHIF,THRDC na PAN-AFRICAN.
Mwenyekiti wa MISA-TAN Salome Kitomari aliyemaliza muda wake akipewa Tuzo ya heshima.
Makamu Mwenyekiti wa MISA-TAN aliyemaliza muda wake James Malenga akipewa Tuzo ya heshima.
Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN aliyemaliza muda wake Idda Mushi akipokea Tuzo ya heshima.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com