Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAKOZI : SHIRECU LAZIMA IJIENDESHE KIDIJITALI NA KIBIASHARA, HATUPASWI KULALAMIKA KILA SIKU

Mrajis Msaidizi wa Vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga, Kakozi Ibrahim akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 30 wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) Ltd.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga, Kakozi Ibrahim, amesisitiza umuhimu wa vyama vya ushirika kuendeshwa kwa mifumo ya kisasa ya kidijitali na kibiashara.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 30 wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU 1984 LTD ), uliofanyika leo katika ukumbi wa SHIRECU,  Ibrahim ameweka wazi kwamba Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) inasisitiza vyama vya ushirika kuwa na akaunti za benki katika benki ya Maendeleo ya ushirika, na kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidijitali kwa ajili ya kuboresha utendaji wa vyama hivyo. 

Amesema mwelekeo wa uendeshaji wa vyama vya ushirika nchini lazima ubadilike ili kutoa nafasi kwa vyama hivyo kujiendesha kibiashara, kuongeza tija, na kuchangia zaidi katika uchumi wa taifa.

"Tunataka kuona vyama vya ushirika vikijiendesha kibiashara, na sio tena kutegemea tu huduma za msingi. Vyama vya ushirika lazima viwe na nguvu na viwe na uwezo wa kufanya biashara ili kusaidia wanachama wao. Mapato yote yanayotokana na vyama vya ushirika ni mali ya umma , wanachama," amesema Ibrahim.

Ibrahim amesema vyama vya ushirika lazima viongeze nguvu katika kuzalisha mazao na kuwekeza katika miradi ya kiuchumi ili kuwa na michango inayokubalika. 

Amehimiza kwamba wanachama wa vyama vya ushirika wasikubali kukaa na kulalamika, badala yake watumie rasilimali walizonazo kuboresha hali zao za kiuchumi.

“SHIRECU imekua kwa muda mrefu, lakini lazima tuondoke kwenye mazoea ya zamani ya kutoshughulika na mazao ya kilimo. Hatupaswi kukaa na kulalamika, tunazo rasilimali na nguvu za kufanya biashara kwa mafanikio," amesema Mrajis Msaidizi huyo.

Akizungumzia ushirikiano na wadau, Ibrahim amesema  vyama vya ushirika lazima vishirikiane na wadau wa kibiashara na wawe na mikakati ya kuzalisha bidhaa na huduma zitakazowawezesha wanachama kupata faida. 

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa vyama vya ushirika kushirikiana na wadau kama washirika na siyo kama wawekezaji.

“Nataka kuona viongozi na wanachama wanaoshirikiana na wengine kama washirika na siyo kama wawekezaji pekee. Vyama vya ushirika vinatakiwa kuwa na nguvu ya kufanya biashara na kuwa na misingi ya kujitegemea,” ameeleza Ibrahim.

Aidha, amesisitiza kuwa hakuna nafasi kwa viongozi au wanachama watakaokwama katika mabadiliko, akieleza kuwa kila mmoja lazima aonyeshe ufanisi katika kushughulika na mazao na kuwa na misingi imara ya kujitegemea.

"Muda wa kulalamika umekwisha. Vyama vya ushirika lazima viwe na mabadiliko ya kweli. Hatutavumilia kiongozi au mwanachama ambaye atasema 'tumezoea hivi.' Hatutaki kuona mtu akizuia maendeleo," ameongeza.

Mkutano huo wa SHIRECU umelenga kuimarisha ushirika kwa kuhimiza mabadiliko ya kimfumo, kuanzisha mifumo ya kidijitali, na kuweka mikakati ya kibiashara ili kutoa manufaa kwa wanachama na jamii kwa ujumla.

 Vyama vya ushirika vimetakiwa kuwa na umoja na kuwa na uwezo wa kufanya kazi kibiashara ili kuleta maendeleo endelevu.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo umejadili, kupokea na kuhuisha sera mbalimbali za Union, kujadili na kupitisha ukomo wa madeni, kupokea taarifa ya utekelezaji ya bodi ya SHIRECU na kupitisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka 2025/2026 ambayo ni  shilingi 2,729,477,473/=.

Mrajis Msaidizi wa Vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga, Kakozi Ibrahim akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 30 wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) Ltd uliofanyika leo Machi 28,2025 katika ukumbi wa SHIRECU kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ili kuimarisha ushirika. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga, Kakozi Ibrahim akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 30 wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) Ltd uliofanyika leo Machi 28,2025 katika ukumbi wa SHIRECU kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ili kuimarisha ushirika.

Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 30 wa SHIRECU, Yohana Maganga akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 30 wa SHIRECU, Yohana Maganga akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 30 wa SHIRECU, Yohana Maganga akizungumza kwenye mkutano huo
Asnath Changamike akisoma taarifa ya utekelezaji wa Bodi ya SHIRECU 1984 kwa niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya SHIRECU 1984 LTD, Lenis Kulwa Jishanga
Asnath Changamike akisoma taarifa ya utekelezaji wa Bodi ya SHIRECU 1984 kwa niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya SHIRECU 1984 LTD, Lenis Kulwa Jishanga
Mwenyekiti wa bodi ya SHIRECU 1984 LTD, Lenis Kulwa Jishanga akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 30 wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) Ltd
Mwenyekiti wa bodi ya SHIRECU 1984 LTD, Lenis Kulwa Jishanga akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa 30 wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU (1984) Ltd

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com