Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTOTO HUYU ANAHITAJI MATIBABU AMEMEZA UFUNGUO WA KUFULI

Mama mzazi wa mtoto, mwenye umri wa mwaka mmoja, anaomba msaada wa matibabu kwa mtoto wake ambaye anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuondoa ufunguo alioumeza.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Naomi John, mkazi wa Majengo ya Zamani, Kata ya Kambarage, Manispaa ya Shinyanga, anasema kwamba tarehe 27 Februari 2025, mwanae alimeza ufunguo wa kufuli. 

Alimpeleka mtoto wake katika Kituo cha Afya Kambarage ambapo alipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Baada ya kufika hospitalini, mtoto alifanyiwa vipimo vya X-ray na madaktari walibaini kuwa ufunguo wa kufuli la Solix upo kwenye utumbo mpana. Madaktari walisema kuwa ufunguo huo unaweza kutoka kwa mtoto mwenyewe, lakini mpaka sasa haujatoka. Ili ufunguo huo utolewe, inahitaji upasuaji ambapo gharama zake ni shilingi 750,000/- katika Hospitali hiyo. 

Hata hivyo, Naomi hana uwezo wa kifedha wa kumudu gharama hizo yupo tu nyumbani mtoto hajapata huduma.

Naomi anatoa wito wa msaada ili mtoto wake apatiwe huduma ya upasuaji na kufanyiwa matibabu kwa kuondolewa kwa ufunguo huu hatarishi.

KATAMBI ACHUKUA HATUA ZA HARAKA KWA MTOTO ALIYEMEZA UFUNGUO WA KUFULI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com