
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Kagera Hamimu Mahmudu Omary
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Kagera Hamimu Mahmudu Omary
Na Lydia Lugakila- Bukoba
Makamu Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa Mhe, Stephen Masato Wasira anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu Mkoani Kagera lengo likiwa ni kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kusikiliza kero mbali mbali zinazowakabili Wananchi wa Mkoa wa na kuzitatua.
Akizungumza na vyombo vya habari Machi 19, 2025 katika Ofisi za chama cha mapinduzi zilizopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa huo Hamimu Mahmudu Omary amewaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo ambaye kwa Kagera ni ziara yake ya kwanza akiwa na wadhifa huo wa Makamu Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Tanzania Bara.
Hamimu amesema kuwa Mhe,Wasira atapokelewa machi 22,2025 katika uwanja wa ndege wa Bukoba mnamo majira ya saa tano asubuhi hadi saa tano na nusu asubuhi ambapo atasaini vitabu katika Ofisi za chama hicho kisha saa nane mchana ataelekea Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba katika kata ya Kemondo eneo la ofisi za KCU na kufanya mkutano mkubwa wa hadhara na Wananchi wa Halmashauri hiyo pia Wanakagera kwa ujumla.
"Niwaombe Wananchi mjitokeze kwa wingi tumpokee kiongozi wetu mkubwa" amesema Hamimu.
Hamimu akielezea ziara hiyo amesema kuwa Mhe,Wasira mnamo Machi 23,2025 atakwenda wilaya ya Karagwe ambapo atakuwa na mkutano mkubwa wa ndani atazungumza na Wananchi, Wanachama na viongozi wa chama cha mapinduzi CCM na machi 24 ataingia Wilaya ya Ngara na kuzungumza pia na Wananchi wa Wilaya hiyo viongozi wa chama na Wanachama wenyewe kupitia mkutano wa ndani.
Aidha ameongeza kuwa kiongozi huyo mkubwa atahitimisha ziara hiyo Machi 25, 2025 mjini Bukoba ambapo atafanya majumuhisho lengo na shabaha ikiwa ni kuimarisha chama kuzungumza na kusalimiana na Wanachama wa chama hicho
Social Plugin