Na Lydia Lugakila -Bukoba
Semina hiyo imewakutanisha washiriki 180 kutoka Bukoba Mjini, wakiwemo viongozi wa masoko kutoka kata za Kashai, Rwamishenye, Bakoba Custom, Nyakanyasi, na Soko Kuu.
Semina hiyo imewakutanisha pia wawakilishi wa wauzaji wa mboga mboga, matunda, na samaki ambapo
vongozi wa serikali kutoka mitaa na kata zenye masoko, pamoja na maafisa wa idara za afya, lishe, kilimo, na mifugo kutoka Manispaa ya Bukoba, wamehudhuria ili kupata uelewa wa pamoja kuhusu masuala ya usalama wa chakula.
Semina hii inalenga kuimarisha mifumo ya chakula salama kwa maendeleo ya jamii!
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Agrithaman Mbunge wa Viti Maalum Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayetokana na NG,o Neema Rugangira akifungua mafunzo juu ya maswala ya usalama wa Chakula aliwaambia washiriki kuwa mafunzo hayo yametokana na kufanya ziara katika masoko na kuona namna ambavyo wauzaji wa mboga mboga na vyakula vya nafaka wanavyohifadhi vyakula isivyo salama hivyo shirika likawashirikisha wadau ambao wanaweza kutoa elimu bora juu ya kuhifadhi vyakula na mboga mboga.
“Tumekuwa tukila chakula Kila siku na matunda lakini kama hatuwezi kuhifadhi vizuri chakula ni kazi bure lengo la mafunzo haya ni kuandaa mabalozi bora ambao wanaweza kutumika kuwafundisha wananchi wote namna nzuri ya kuhifadhi chakula na kujua ni kwa jinsi gani wananchi wanaweza kitambua chakula na matunda yaliyoribika ili yasitumike na kuondoka changamotoo za kiafya hasa kansa na vifo ndio maana tumechukua viongozi katika masoko yote ya Bukoba na viongozi wa kata zote 14”, amesema Lugangira.
Amewaambia washiriki wote kuwa kwa kuwa bado ni kiongozi wa Bukoba kupitia uongozi na wadau mbalimbali anafanya jitihada kama kiongozi kuhakikisha Bukoba mjini inakuwa mfano wa kuingwa katika usalama wa chakula kwenye masoko yao.
Reticia Ishengoma ofisa wa maswala ya sera na chakula kutoka Shirika la Kimataifa la GAIN amesema kuwa shirika hilo lilishafanya utafiti na kugundua kuwa wananchi wengi wa Tanzania wanaopata magonjwa ya kansa yanayotoka na uhifadhi mbaya wa vyakula wanatokea Kanda ya Ziwa ikiwemo mkoa wa Kagera hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini kwa njia wanazotumia kuhifadhi chakula.
Amesema katika masoko matano ambayo ameyapitia Bukoba mjini alikuta baadhi ya wauza matunda na mboga mboga wakitumia dawa katika bidhaa na bidhaa hizo zikiendelea kuuzwa sokoni huku akisema kuwa vyakula vingi vya nafaka kama mahindi na Karanga vinavyouzwa sokono viko hatarini kupata Sumu kuvu kwa asilimia kubwa kwani njia inayohifadhi bidhaa hizo sio salama.
Aidha Katibu tawala wa Wilaya ya Bukoba Proscovia Mwambie amesema kuwa kupitia ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kusaidia na viongozi walipata mafunzo haya wataweka utamaduni wa kutembelea masoko na kutoa elimu kwa wananchi juu ya kutambua vyakula vilivyoharibika na jinsi ya kuhifadhi vyakula kwa usalama ili kujenga kizazi bora.
Mafunzo hayo yalitoa fursa kwa washiriki kueleza changamoto za kuhifadhi vyakula na namna bora lakini pia washiriki walifundishwa madhara makubwa yatokanayo na matumizi ya vyakula ambavyo havijahifadhiwa vizuri na jinsi ya kuepuka ikiwemo kuboresha lishe za watoto wao kupitia vyakula vyao.
Social Plugin