Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA NBC TANGA YAKABIDHI BASI KWA TIMU YA COASTAL UNION


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

TIMU ya Coastal Union ya Jijini Tanga imepata ufumbuzi wa muda mrefu wa changamoto ya usafiri baada ya kupatiwa mkopo wa basi wenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 280 kutoka Benki ya NBC.

Akiongea katika hafla ya makabidhiano ya basi hilo mkuu wa Wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye amesema hatua moja ya maendeleo katikaka timu inaletwa miundombinu bora ya kimichezo, mazingira bora ya kifedha kwa wachezaji.

Amesema timu hiyo ina nafasi ya kusababidha mabadiliko chanya katika timu na kufanya kuwa timu bora zaidi nchini lakini pia Afrika kwasababu inawezekana ukitegemea na nidhamu ya wachezaj bila kujali mazingira waliyonayo.

"Tuwatake sasa, tunapoitaja Coastal Union tunataja mabalozi wa Tanga, ndiyo timu pekee inayotutambulisha popote pale Tanzania, tunaweza kuongezea namba ya washabili na sisi kuwa na timu inayowapa Wanatanga na Watanzania furaha,

"Kwahiyo niwatakie kila la kheri, leo tumepiga hatua moja mbele, basi hatua hii tuifurahie kwa matokeo na siyo kwa sababu tu, bali kwa kutuletea matokeo mengine yaliyo bora zaidi", amesema.

Naye Mkurugenzi wa Biashara Benki ya NBC Elvis Ndunguru  amesema benki hiyo imewekeza kiasi cha shilingi Bilioni 32.6 katika Premier Ligi, lakini vile vile katika uwekezaji wa mabasi katika vilabu mbalimbali imefikisha kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 wakati timu hiyo ikiwa ni ya nne kuchukua basi hilo.

Ndunguru amesema NBC itaendelea kutoa udhamini maeneo mengine mbalimbali ambapo sasa wanaokwenda kuangalia uwekezaji wa miundombinu ya viwanja, kwani ni muhimu sana katika kuendelea kudumisha ligi ndani ya nchi.

"Lakini kuna eneo la bima ambapo tumekuwa tukitoa wachezaji na sasa tutazifanya kuwa bora zaidi, lakini huduma za kadi kwa timu mbalimbali, tunajua tayari kuna vilabu kubwa tunatoa kadi za pamoja,

"Kadi hizi zinasaidia pia kuboresha mapato ya vilabu, na hili ni jambo ambalo tunategemea kulipanua kwenda kwenye vilabu vingine ikiwemo Coastal ya hapa Tanga" ,amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com