Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKULIMA WA KAHAWA MBINGA WANUFAIKA NA MBOLEA ZA RUZUKU

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Kahawa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Michael Kanduyu kulia,akimuonyesha Kaimu Meneja wa Chama hicho Farja Komba kushoto,wakikagua miti ya kahawa inayoendelea kuzaa  wakati wa ziara ya kutembelea Wakulima wa kijiji cha Malindindo Halmashauri ya Wilaya Mbinga ,ziara hiyo ililenga kusikiliza changamoto zinazowakabili Wakulima wa zao hilo.
Kaimu Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Kahawa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma (Mbifacu)Faraja Komba na Mwenyekiti wa Chama hicho Michael  Kanduyu (kulia) wakiangalia uzalishaji wa kahawa kwenye shamba la mkulima katika kijiji cha Malindindo kata ya Mhekela Wilaya ya Mbinga


Na Regina Ndumbaro Mbinga .

Wakulima wa kahawa katika Wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, wameishukuru serikali kwa mpango wa kutoa pembejeo za ruzuku katika msimu wa kilimo wa 2023/2024 na 2024/2025. 

Mpango huo umehamasisha wakulima wengi kufufua mashamba yao na kuongeza uzalishaji wa zao hilo. 

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Kahawa Mbinga (Mbifacu), Michael Kanduyu, amesema kuwa ruzuku kwenye mbolea imeongeza uzalishaji kwa kasi kubwa, kwani wakulima sasa wanapata mbolea kwa bei nafuu ukilinganisha na miaka iliyopita.

Kwa mujibu wa Kanduyu, mbolea ya UREA inauzwa kwa Sh. 68,000, CAN kwa Sh. 62,000 na SA kwa Sh. 48,000, tofauti na awali ambapo bei ilikuwa kati ya Sh. 150,000 hadi Sh. 180,000 kwa mfuko mmoja. 

Hali hii imerahisisha uzalishaji wa kahawa, huku wakulima wakipata faida zaidi. 

Hata hivyo, Kanduyu ameomba serikali kutoa ruzuku pia kwa dawa za kupulizia kahawa, kama inavyofanyika kwenye zao la korosho na pamba, ili kupunguza gharama za uzalishaji.

Lucas Mahay, mkulima kutoka Kijiji cha Malindindo, amesema kuwa kabla ya mpango wa ruzuku, wakulima wengi walipunguza ukubwa wa mashamba yao kutokana na gharama kubwa za pembejeo. 

Ameeleza kuwa mpango wa pembejeo za ruzuku umewasaidia wakulima kurejesha matumaini na kupanua mashamba yao. 

Pia, amezisifu juhudi za viongozi wa Mbifacu kwa kuanzisha mpango wa kukopesha wakulima mbolea, ambao umeongeza ushiriki wa wakulima wengi katika vyama vya ushirika.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mbifacu, Faraja Komba, amesema kuwa uzalishaji wa kahawa umeongezeka kutoka wastani wa tani 15,000 msimu wa 2021/2022 hadi tani 25,000 msimu wa 2024/2025. 

Ongezeko hili limeongeza mapato ya wakulima na kuchangia katika pato la serikali kupitia ushuru na tozo mbalimbali. 

Ameongeza kuwa vyama vya ushirika vimewekeza katika miradi ya maendeleo kama mashamba, vyombo vya usafiri na maghala ya kuhifadhi kahawa.

Komba pia ameeleza kuwa soko la kahawa limepanuka kwa wakulima kupitia masoko matatu makuu: soko la minada, soko la moja kwa moja, na soko la mkataba. 

Masoko haya yameongeza ushindani na kutoa fursa kwa wakulima kupata bei nzuri ya kahawa. 

Aidha, amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Mbifacu imetoa zaidi ya Sh. milioni 999 kwa halmashauri za wilaya ili kuboresha huduma za kijamii kupitia mapato yatokanayo na zao la kahawa.

Katika msimu wa kilimo wa 2024/2025, wakulima wamelipwa zaidi ya Sh. bilioni 208 baada ya kuuza tani 23,000 za kahawa, huku bei ya wastani ikiwa Sh. 8,700 kwa kilo.

 Katika baadhi ya maeneo, kahawa iliuzwa kwa kati ya Sh. 9,000 na 10,000 kwa kilo, hali iliyoongeza kipato cha wakulima na kuimarisha uchumi wao. 

Komba ameeleza kuwa Mbifacu pia imetoa mikopo ya pembejeo yenye thamani ya Sh. bilioni 1.2 kwa wakulima, ambayo italipwa kupitia vyama vya msingi vya ushirika (Amcos).

Afisa Masoko wa Mbifacu, Osmund Mbunda, amesema kuwa chama hicho kinasimamia masoko matatu muhimu ya kahawa. 

Ametaja soko la awali, ambapo mkulima huuza kahawa isiyochakatwa, soko la moja kwa moja ambapo mkulima huuza kahawa safi, na soko la mnada huku akifafanua kuwa soko la moja kwa moja lina faida

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com