Na Neema Paul - Kahama
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Mhe. Mboni Mhita amekiomba chama cha ushirika KACU wilayani humo kuwahimiza Wakulima kukata Bima ya zao la Bamba na Tumbaku ili kuondokana na hasara ambayo imekuwa ikitokea kutoka na mabadiliko ya Tabia ya Nchi .
Hayo ameyasema leo katika Mkutano Mkuu wa 29 wa Mwaka wa KACU uliofanyika katika ukumbi wa KACU uliopo Mhongolo Jineri na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka halmashauri ya Ushetu,Msalala na Manspaa ya Kahama ,ambapo amesema mabadiliko ya Tabia ya Nchi yamepelekea Ushirika kushindwa kufikia malengo ya uzalishaji kwa msimu wa kilimo 2024/2025 kutokana na hali ya hewa.
" Sasa hivi tupo kwenye mabadiliko ya Tabia ya Nchi kwa mwaka Jana mazao yetu yaliathiriwa na mvua ya mawe ,lakini pia kuna ukame tusilime kwa kutegema mvua hivyo kuwa na Bima kwa mkulima itawasaidia kufidia gharama zenu,kingine jitahidini kurejesha mikopo kwenye hizi huduma za kifedha ili na wengine wakope na kukuza mitaji yetu ya kilimo",amesema
Aidha amelekeza kuwa ushirika unapaswa kuwa na ushirikiano ,kuheshimu taratibu na Sheria zilizowekwa pamoja na kuboresha msingi na ubora wa mazao kuanzia shambani hadi kwa mlaji ili kusaidia kahama kutambulika kimataifa kwa uzalishaji wa mazao ya Pamba na Tumbaku.
Awali Mrajisi wa vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga bwana Kikozi Ibrahimu ameagiza ushirika kuendeshwa kwa njia ya mfumo kuwa na miradi ya kibiashara pamoja na kuepuka migogoro inayotokea ndani ya ushirika kwani hali hiyo itapelekea kuharibu na kuvuruga taswira ya ushirika.
" Wajumbe mnapaswa kuachana na taarifa za makaratasi imepitwa na wakati na hii itasaidia kuondoa undanganyifu,lakini sitasita kumuondoa mtu anayeingia kwenye ushirika kuharibu mahusiano yaliyopo",amesema.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba amemuomba Mwenyekiti wa KACU bwana Emmanueli Nyambi Masanja kuzungumza na wahusika wa pembe jeo kupunguza bei pamoja na. kuunda tume itakayosaidia kufanya utafiti wa mazao mengine mapya ili kusaidia wakulima kulima mazao mengine yatakayoendana na ardhi yetu.
Social Plugin