Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SOUWASA YAADHIMISHA KILELE CHA WIKI YA MAJI KWA KUTAMBULISHA MRADI WA MAJI WA LONDONI, SINAI NA MANG'UA


Kaimu Mkurugenzi wa SOUWASA Mhandisi Japhary Yahaya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sinai Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma katika kilele cha kuadhimisha Wiki ya Maji
Mwenyekiti wa kijiji cha Sinai akishukuru uongozi wa Souwasa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma kwa kuwatatulia kero ya maji ya muda mrefu katika kilele cha wiki ya maji ambayo iliwafikia wana Sinai 
Mwananchi wa kijiji cha London Bi Grace Komba akimshukuru kaimu mkurugenz Mhandisi Japhary Yahaya alipowasili katika kijiji hicho siku ya kilele cha wiki ya maji Manispaa Ya Songea Mkoani Ruvuma
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa SOUWASA Mhandisi Japhary Yahaya siku ya kilele cha maji kijij cha Mang'ui Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma

Na Regina Ndumbaro - Songea

Katika juhudi za kuboresha upatikanaji wa maji safi, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Songea (SOUWASA) imetambulisha mradi mkubwa wa maji katika maeneo ya Sinai na Londoni. 

Mradi huu, wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 1, unalenga kunufaisha wakazi wapatao 5,883 kwa kuboresha miundombinu ya maji na kupunguza adha ya kutafuta maji kwa umbali mrefu.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa mradi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa SOUWASA, Mhandisi Japhary Yahaya, ameeleza kuwa mradi huo utajumuisha uchimbaji wa visima viwili, ujenzi wa tanki lenye uwezo wa lita 200,000, pamoja na ujenzi wa nyumba mbili za pampu na mfumo wa kutibu maji. 

Ameongeza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha wakazi wa Sinai na Londoni wanapata huduma bora ya maji safi na salama, hatua ambayo itaimarisha afya na ustawi wa jamii.

Diwani wa Kata ya Lilambo, Yobo Mapunda, ameipongeza SOUWASA kwa juhudi hizi, akibainisha kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka kwani wakazi wa Sinai wamekuwa wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa maji kwa muda mrefu. 

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Londoni, Selemani Zawamba, amesema kuwa robo tatu ya wakazi wa Londoni walikuwa hawana huduma ya maji safi, hali iliyosababisha changamoto za kiafya, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mlipuko na matatizo ya tumbo.

Wakazi wa Sinai na Londoni wameonyesha furaha yao kuhusu mradi huo na kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza sera ya "Kumtua Mama Ndoo Kichwani." Wameeleza kuwa mradi huu utapunguza hatari ya ajali kwa watoto waliokuwa wakitumbukia kwenye visima na kurahisisha shughuli za kila siku kwa wanawake waliokuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji.

Maadhimisho ya Wiki ya Maji mwaka huu, yaliyoanza Machi 16 na kufikia kilele Machi 22, 2025, yamebeba kaulimbiu: "Uhifadhi wa Uoto wa Asili kwa Uhakika wa Maji." 

Mradi huu wa maji ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji safi kwa urahisi, huku ukiakisi dhamira ya kulinda mazingira na kuimarisha huduma za msingi kwa jamii.

 Londoni, Selemani Zawamba, amesema kuwa robo tatu ya wakazi wa Londoni walikuwa hawana huduma ya maji safi, hali iliyosababisha changamoto za kiafya, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mlipuko na matatizo ya tumbo.

Wakazi wa Sinai na Londoni wameonyesha furaha yao kuhusu mradi huo na kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza sera ya "Kumtua Mama Ndoo Kichwani." 

Wameeleza kuwa mradi huu utapunguza hatari ya ajali kwa watoto waliokuwa wakitumbukia kwenye visima na kurahisisha shughuli za kila siku kwa wanawake waliokuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji.

Maadhimisho ya Wiki ya Maji mwaka huu, yaliyoanza Machi 16 na kufikia kilele Machi 22, 2025, yamebeba kaulimbiu: "Uhifadhi wa Uoto wa Asili kwa Uhakika wa Maji." 

Mradi huu wa maji ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji safi kwa urahisi, huku ukiakisi dhamira ya kulinda mazingira na kuimarisha huduma za msingi kwa jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com