Na Regina Ndumbaro, Ruvuma
Waziri wa Afya na Mbunge wa Songea Vijijini, Mheshimiwa Jenista Mhagama, ametangaza rasmi kuwepo kwa ugonjwa wa Mpox (Murbag) nchini Tanzania na kueleza hatua zinazochukuliwa na serikali ili kukabiliana nao.
Akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Songea Mjini, Waziri Mhagama amewataka wananchi kupata elimu sahihi kuhusu ugonjwa huo, kujikinga na kuepuka maambukizi.
Ameeleza kuwa Mpox ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya kugusana moja kwa moja na mgonjwa, kukumbatiana, kubusiana, pamoja na kutumia vifaa vilivyotumiwa na mtu aliyeambukizwa.
Katika juhudi za kudhibiti ugonjwa huo, Waziri Mhagama amesema kuwa serikali imejipanga kikamilifu na imeandaa kampeni maalum ya siku 54 za mapambano dhidi ya Mpox.
Aidha, ameeleza kuwa mnamo Machi mwaka huu, kulikuwa na tetesi za uwepo wa wagonjwa wenye dalili za Mpox mkoani Kagera, na kufikia Machi 9, 2025, serikali ilithibitisha rasmi kuwa na wagonjwa wawili wa ugonjwa huo.
Amehimiza wananchi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa usafi wa mwili na mazingira kama moja ya njia za kujikinga na maambukizi.
Mbali na mapambano dhidi ya Mpox, Waziri Mhagama ameweka wazi kuwa serikali inaendelea kufanya juhudi kubwa za kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2030, lengo la serikali ni kuhakikisha vifo vya akina mama na watoto vinapungua kwa kiasi kikubwa na kila mama anapata haki yake ya msingi ya kiafya.
Ameeleza kuwa serikali inachukua hatua madhubuti za kuimarisha sekta ya afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya kote nchini.
Aidha, serikali imeendelea kuboresha huduma za afya ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora kwa wakati.
Katika hotuba yake, Waziri Mhagama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuimarisha sekta ya afya nchini.
Amebainisha kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia, serikali imefanikiwa kuboresha huduma za afya kwa kiwango kikubwa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vipya vya afya na upatikanaji wa dawa muhimu.
Serikali inaendelea kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na wataalam wa afya katika mapambano dhidi ya Mpox na magonjwa mengine yanayoathiri jamii.
Wananchi wanahimizwa kuwa waangalifu, kuzingatia usafi wa mwili na mazingira, na kufuata maelekezo ya wataalam wa afya ili kuhakikisha afya bora kwa wote.

Social Plugin