


Na Regina Ndumbaro, Ruvuma
Amesema mkoa huo ulikuwa mwenyeji wa Tamasha la Taifa la Tatu la Utamaduni pamoja na maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwa mafanikio makubwa.
Aidha, amewapongeza viongozi wa mkoa, wataalamu, na wananchi kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha matukio hayo ya kitaifa.
Katika kikao hicho, Kanali Ahmed amepongeza viongozi wa Chama na Serikali, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na viongozi wa taasisi za umma na binafsi kwa ushirikiano wao katika kusimamia utekelezaji wa majukumu ya maendeleo ya mkoa.
Amesisitiza kuwa serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, hususan katika sekta za elimu, afya, maji, barabara, nishati, kilimo, na miundombinu mingine, ikiwemo uboreshaji wa bandari.
Mkoa wa Ruvuma umeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, ambapo kwa mwaka wa fedha 2023/24, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani humo imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 20.33, sawa na asilimia 117% ya lengo la makusanyo ya bilioni 17.43.
Kwa upande wa halmashauri, jumla ya shilingi bilioni 31.46 zimekusanywa, sawa na asilimia 112.85 ya lengo la kukusanya bilioni 27.88.
Mkuu wa Mkoa amepongeza juhudi za TRA, viongozi wa halmashauri, na wafanyabiashara kwa kulipa kodi kwa hiari, jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya ndani.
Katika sekta ya kilimo, mkoa umeendelea kufanya vizuri ambapo kwa msimu wa 2023/24 umezalisha tani milioni 1,955,763.76 za mazao ya chakula, huku mahitaji halisi ya mkoa yakiwa tani 470,000.
Hii imesababisha ziada ya tani milioni 1,485,763.76, ambazo huuzwa ndani na nje ya mkoa, na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima.
Mafanikio haya yanatokana na mpango wa pembejeo za ruzuku unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia, ambapo kwa msimu wa 2023/24, tani 113,000 za mbolea zilitumika, huku kwa msimu wa 2024/25 hadi kufikia Januari, tani 55,488.886 zilikwishatumika.
Mkuu wa Mkoa ameendelea kueleza kuwa Ruvuma imeimarika katika miundombinu, biashara, na uwekezaji, hususan katika uchimbaji wa madini kama makaa ya mawe.
Aidha, mkoa umeshuhudia maboresho ya uwanja wa ndege wa Songea na kuimarika kwa usambazaji wa umeme, ambapo vijiji 541 kati ya 551 vimeunganishwa na umeme, sawa na asilimia 98.18.
Katika sekta ya elimu, miundombinu imeboreshwa, na kwa mwaka 2023/24, wanafunzi 27,281 waliofaulu darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, huku wanafunzi 41,662 wakiandikishwa elimu ya awali, sawa na asilimia 82.12 ya lengo la wanafunzi 46,707.
Mkoa umeendelea kuhakikisha elimu bora kwa wote kwa kuongeza miundombinu na rasilimali muhimu za kujifunzia.
Social Plugin