
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Bw. Shaibu Ndemanga, akihutubia walimu kwenye mkutano mkuu wa Chama cha walimu wilaya ya Bagamoyo

Katibu wa Chama cha walimu wilaya ya Bagamoyo, Mwalimu Joyce Maisa

Mwenyekiti kitengo cha walimu wanawake CWT, mwalimu Veronica Kirumbi akimshukuru mgeni rasmi kwa hotuba .

Katibu wa Chama cha walimu mkoa wa Pwani, Bi. Suzan Shesha akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa CWT Wilaya ya Bagamoyo
****
NA. ELISANTE KINDULU, BAGAMOYO.
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo ,Shaibu Ndemanga amewataka maafisa utumishi na wakuu wa idara katika halmashauri za Bagamoyo na Chalinze kuwahudumia vizuri walimu bila ya kuwazungusha.
Mkuu wa wilaya aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Chama cha walimu wilaya ya Bagamoyo leo, tarehe 18.3.2025 latika ukumbi wa Stella Maris mjini hapa.
Bw. Ndemanga amesema hawezi kuwavumilia viongozi wasiojali shida za watumishi hususani walimu.
Aidha mkuu wa Wilaya amewaasa walimu kufanya kazi kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu .
" CWT ni chama cha kuwatetea walimu, Lakin niwaombe viongozi wa Chama msitetee walimu wanaokengeuka kupita kiasi. Kuna wakati kulikuwa na mwalimu alikuwa na changamoto. Mwalimu yule hata alipojaribu kutetewa na chama bado aliwadharau na kujiona anaweza kujijitetea peke yake", alisema Ndemanga.
Naye katibu wa CWT Wilaya ya Bagamoyo Mwalimu Joyce Maisa katika risala ya kamati ya utendaji ya wilaya alizitaja changamoto kadhaa zinazowakabili walimu wilaya ya Bagamoyo.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kwa baadhi ya viongozi wanaowahudumia walimu kutokuwa na lugha nzuri kwa walimu, ucheleweshwaji wa fedha za likizo na walimu hodari kutokupewa zawadi zao kwa wakati.
Akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza, Mwenyekiti wa Chama hicho wilaya ya Bagamoyo Mwalimu Hamisi Kimeza aliishukuru serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka kliniki inayotambulika kwa Jina la kliniki ya mama Samia inayotembea nchi nzima kusikiliza na kutatua kero za walimu.
Social Plugin