Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasira akitoa Nasaha kwa viongozi wa Jeshi la Jadi Sungusungu.
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara Stephen Wasira,amekabidhi Pikipiki mpya kwa Jeshi la Jadi Sungusungu wilaya ya Shinyanga,ambayo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobasi Katambi.
Amekabidhi Pikipiki hiyo Machi 26,2025 akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, uhai wa Chama na kusikiliza changamoto za wananchi mkoani Shinyanga.
Amempongeza Mbunge Katambi kwa kutoa Pikipiki hiyo, huku akilisihi Jeshi hilo la Jadi Sungusungu, kwamba liendee kufanya kazi ya kudumisha amani ya nchi.
“Usafiri huu utumieni vizuri katika kuendelea kudumisha amani ya nchi,”amesema Wasira.
Naye Mbunge Katambi, ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu, amesema ametoa Pikipiki hiyo ili kuwapatia usafiri viongozi jeshi hilo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Mwenyekiti wa Sungusungu John Kadama ameshukuru kwa usafiri huo ambao utasaidia katika shughuli zao za kulinda amani na utulivu.
TAZAMA PICHA👇👇
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Stephen Wasira akikabidhi Kadi ya Pikipiki kwa viongozi wa Jeshi la Jadi Sungusungu.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi akiwa na viongozi wa Sungusungu katika picha.
Muonekano wa Pikipiki mpya SanLG ambayo wamepewa Jeshi la Jadi Sungusungu na Mbunge Katambi.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga akiwa kwenye mkutano .
Social Plugin