
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeshiriki katika kongamano la wadau wa habari nchini Tanzania lililoendeshwa na MISA-Tanzania katika hoteli ya Morena, Jijini Dodoma, Tanzania.
THRDC imewakilishwa na Mkuu wa Idara ya Utetezi Wakili Paul Kisabo ambaye ameshiriki katika mdahalo kwenye kongamano hilo na kuwasilisha kuhusu wajibu na mchango wa THRDC katika kulinda na kutetea waandishi wa habari na sekta ya habari nchini hasa wakati wa uchaguzi.
Mchango wa THRDC katika sekta ya habari hasa wakati wa uchaguzi ni pamoja na kufanya uchambuzi wa Sheria na Kanuni za uchaguzi na kuwasilisha maboresho kwa mamlaka, kuendesha kesi mkakati zinazohusu sheria za waandishi wa habari, kufanya mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu haki na wajibu wa waandishi wa habari wakati wa uchaguzi lakiki pia mafunzo kwa makamanda wa Jeshi la Polisi kuhusu wajibu wao wakati wa uchaguzi ikiwemo kuzingatia haki za waandishi wa habari wakati wa uchaguzi, n.kz.
Washiriki wa kongamano hilo ni pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya habari nchini.
Imetolewa na THRDC
14.03.2025
Dodoma, Tanzania




Social Plugin