Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HAKUNA WA KUSHINDANA NA DKT. SAMIA KATIKA UCHAGUZI WA 2025- MNEC NDELE MWASELELA


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Ndugu Ndele Mwaselela, amewaambia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa kazi nzuri zinazofanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka minne, katika sekta mbalimbali, zimewafanya wananchi wa Tanzania kumpenda na kumwamini Dkt Samia Suluhu. Kila tunapopita, wananchi wana imani kubwa na Rais Samia.

Ndugu Mwaselela amewaomba Watanzania wote, kutoka bara na visiwani, kumpigia kura nyingi Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wa udiwani na wabunge kupitia CCM.

"Twendeni tukaionyeshe dunia kuwa tuna Rais bingwa wa kuleta maendeleo kwa wananchi wote. Tuweke wazi kuwa tuna Dkt Samia Suluhu Hassan, ambaye ni bingwa wa diplomasia na bingwa wa demokrasia ya kweli. Kwa namna alivyomchapa kazi, hatuna mwingine wa kumshinda. Mgombea wetu ni Dkt Samia Suluhu Hassan, na mgombea mwezake ni Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi",amesema MNEC huyo.

Wito huu ameutoa wakati wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Ndugu Stephen Wasira, katika Mkoa wa Kagera.

#Kazi na Utu, Tunasonga Mbele

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com