
Wananchi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Mchoteka waliojitokeza kumsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho Wilayani Tunduru

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho akizungumza na Wananchi na Wanachama Kata ya Marumba Wilaya Tunduru


Wananchi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Mchoteka waliojitokeza kumsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho Wilayani Tunduru

Wananchi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Nalasi Wilayani Tunduru wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho
Na Regina Ndumbaro Tunduru.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, ameendelea na ziara yake ya kata kwa kata katika Wilaya ya Tunduru, akitembelea Kata ya Marumba, Mchoteka, na Nalasi, zilizopo Jimbo la Tunduru Kusini.
Ziara hiyo imelenga kuimarisha mshikamano ndani ya chama na kusikiliza kero za wananchi.
Akizungumza leo tarehe 23 Machi, Oddo amewataka viongozi kushirikiana na wananchi kwa karibu na kuhakikisha hakuna mgawanyiko ndani ya chama.
Katika hotuba yake, Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa wanaowania nafasi za uongozi wasiwatishe wenzao, bali waachie wananchi kufanya maamuzi yao kwa uhuru.
Amewataka viongozi na wanachama wa CCM kudumisha mshikamano, uadilifu, na kufuata taratibu za chama ili kuhakikisha chama kinabaki imara.
Pia amewataka kuendeleza juhudi za kusaka kura nyingi kwa Rais Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa CCM katika chaguzi zijazo.
Wananchi wamepata fursa ya kuuliza maswali, ambapo Najali Silaju kutoka Kata ya Mbati ameeleza kuwa Bodi ya Korosho inachangia kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo, huku pembejeo za ruzuku zikichelewa kufika kwa wakati.
Rashid Msenga ameiomba serikali iboreshe miundombinu ya barabara, hasa ujenzi wa daraja la Mtiti linalounganisha Marumba na Mbati.
Dalia Baina Mkoela kutoka Kata ya Nalasi ameeleza changamoto ya shule ya msingi Lipepo, ameyataja madarasa, vyoo, na nyumba za walimu, huku akilalamikia ukosefu wa umeme na maji katika kituo cha afya cha eneo hilo.
Akijibu hoja hizo, Afisa Mtendaji wa Kata, Ramadhan Issa Mandingo, amekiri changamoto zilizotajwa na kueleza kuwa miradi ya maji iko chini ya mkandarasi na inatarajiwa kukamilika.
Kuhusu ujenzi wa vyoo, amesema kuwa umeanza lakini bado haujakamilika.
Pia ameeleza kuwa jitihada zinaendelea kuhakikisha huduma za umeme na miundombinu ya shule zinaboreshwa.
Ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma inaendelea katika kata mbalimbali za Wilaya ya Tunduru, huku akihimiza mshikamano ndani ya chama na serikali ili kuimarisha maendeleo ya wananchi.
Social Plugin