Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHADEMA YAWAALIKA CCM KUUNGANA NAO KUFANYA MAANDAMANO KUPINGA MATUKIO YA UTEKAJI

 Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga.

Na Mwandishi wetu - Shinyanga

Kufuatia Matukio mawili yanayodaiwa kuwa ya utekaji kwa makada wa CCM na Chadema, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEM) Kanda ya Serengeti kimesema kimeandaa maandamano ya amani ili kupinga ukiukwaji haki za binadamu. 

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Serengeti Jackson Mnyawami amelaani vitendo vya utekaji uliotokea kwa viongozi wa CCM na Chadema katika kanda ya Serengeti inayounganisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga. 

Akizungumza leo Machi 29, 2025 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ya kanda maalum ya Chadema Mnyawami amesema kuwa vitendo vya utekaji vinavyoendelea vimeleta hofu kubwa na wasiwasi kwa wananchi,

“Matukio hayo mawili yalihusisha kiongozi wa hamasa katika jimbo la Tarime vijijini Mussa Juma (Tall) na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Daniel Chonchorio ambaye ni mtia nia jimbo la Tarime mjini, utekaji huu unaweka wasiwasi mkubwa miongoni mwa wananchi” amesema Mnyawami. 

“Pamoja na Jeshi la polisi kukanusha katika taarifa zao wamekanusha kujua watu hao walipo, tunaamini wanapaswa kuwajibika kutokana na jukumu la kisheria waliopewa kuhakikisha upatikana wa watu hao” amesema Mnyawami.

Mnyawami ameelekeza  CHADEMA mkoa wa Mara kuanza kuratibu maandamano ya amani kwa madhumuni ya kupinga ukatili wa haki za binadamu, yatakay hudhuriwa na viongozi wote pamoja na wanaCCM wanaalikwa kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu,

“Tunaelekeza mkoa wa Mara kuanza kuratibu maandamano ya amani ambayo yatahudhuriwa na viongozi wa kanda, pia waanze kutoa taarifa polisi na lengo kubwa ni kupinga utekaji unaoendelea mkoani Mara na tunawakaribiasha wanaCCM wote ambao ni waathiriwa wa utekaji kupaza sauti zao” Mnyawami. 

Hivyo basi kutokana na matukio hayo Chadema Kanda ya Serengeti wamesisitiza serikali juu ya mambo kadhaa ili kurejesha amani ambayo imetoweka kwa wananchi, pamoja na kurejesha imani ya wananchi ambayo imetoweka juu ya jeshi la polisi. 

“Tunaomba jeshi la polisi kuwajibika kwa kushindwa kulinda usalama wa raia, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aunde tume ya kijaji kuchunguza matukio ya utekaji na kuharakisha utekelezaji wa ripoti ya haki jinai ambayo ilionesha vyombo vya ulinzi na usalama kuvunja kwa haki za binadamu” amesema Mnyawami. 

“Tunawasihi wadau wa haki za binadamu na wananchi kupaza sauti dhidi ya vitendo viovu, tunaunga mkono viongozi wa chama mkoa wa Mara kukutana na viongozi wa dini kuwaeleza umuhimu wa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na idadi ya wananchi waliouwawa”, amesema Mnyawami.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com