Mwanamke mwenye ualbino aliyefahamika kwa jina la Wande Mbiti (38) amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake alipokuwa akiishi maeneo ya Nhelegani kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga huku mlango wa nyumba yake ukiwa umefungwa kwa kufuli kwa nje.
Tukio hilo limetokea Machi 02, 2025 katika Kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Inaelezwa kuwa majira ya mchana majirani zake Wande Mbiti walisikia harufu kali wakati wakichuma mboga katika moja ya shamba lililopo jirani na nyumba yake iliyokuwa imefungwa kwa nje ndipo waliita viongozi wa kijiji na mtaa na kulitaarifu jeshi la polisi lililofika na kuvuja mlango na kukuta maiti ya Wande Mbiti ikiwa kitandani.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga ACP. Kennedy Mgani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kubaini sababu ya kifo chake.
Social Plugin