Habari Mpya

    Loading......

JUMBE AAHIDI KUTOA KIBUNDA ENDAPO STAND UNITED ITAICHAPA MTIBWA SUGAR DIMBA LA CCM KAMBARAGE

Mdau wa michezo mkoani Shinyanga ,Jackline Isaro akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa timu ya Stand United dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Machi 17,2025 uwanja wa CCM Kambarage.

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mhandisi James Jumbe Wiswa, Mdau mkubwa wa michezo, ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa timu ya Stand United FC iwapo itaifunga timu ya Mtibwa Sugar FC ,katika mchezo utakaozikutanisha timu hizo na kupigwa Machi 17,2025 katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Machi 14, 2025,Mjini Shinyanga  Shinyanga, Mdau wa michezo ,Jackline Isaro, amesema kuwa Motisha hiyo imeahidiwa kutolewa na Mhandisi James Jumbe Wiswa kama sehemu ya juhudi za kuendeleza michezo mkoani Shinyanga na kuhakikisha timu ya Stand United inafanya vizuri ili iweze kutoka hatua ya Champion Ship na kurejea Ligi kuu hali itakayosaidia kurejesha heshima ya timu ya Stand United FC 'Chama la Wana'.

Jackline amefafanua kuwa Mhandisi Jumbe, ambaye ni mkazi wa Shinyanga na mpenzi wa michezo, ameonyesha dhamira yake ya dhati kwa kuhamasisha wachezaji wa timu ya Stend united na mashabiki wa timu hiyo kwenda kuipa hamasa timu yao katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga Machi 17 .

Aidha, Jackline amesema Mhandisi James Jumbe ametangaza kununua tiketi 100 kwa mashabiki wa timu ya Stand United FC ili waweze kuingia bure uwanjani huku zoezi la kutoa motisha kwa kila goli litakalofungwa na Stand United katika mchezo huo kwa kutoa shilingi 200,000 kwa kila goli.

"Mhandisi James Jumbe Wiswa ameichukulia kwa uzito mechi hii kati ya Stand United FC na Mtibwa Sugar FC, kwa kuwa yeye ni mkazi wa Shinyanga pia ni mwanamichezo kwamba endapo timu itashinda na kupata pointi tatu, atatoa zawadi ya shilingi milioni mbili . Pia motisha ya shilingi 200,000/= ambayo ameendelea kutoa kwa kila goli litakalofungwa na timu ipo pale pale," amesema Jackline.

Jackline amewahimiza wananchi wa mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao, Stand United FC ili iweze kupata pointi 3 muhimu katika uwanja wake wa nyumbani kwa kuibamiza timu ya Mtibwa Sugar.

"Tunataka kurudisha heshima ya mkoa wa Shinyanga kwa kuiinua timu hii inayodhaminiwa na Jambo Group kwa kuiwezesha timu ya Stend ," amesisitiza Jackline.

Kwa upande wake Afisa Habari wa timu ya Stand United FC, Ramadhani Zoro akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa motisha iliyo tolewa na Mhandisi Jumbe pamoja na jambo Group itachangia katika kushinda mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar FC.

"Tunamshukuru Mhandisi Jumbe kwa motisha hii kuahidi shilingi milioni 2 iwapo timu itashinda na tiketi 100 kwa mashabiki watakao ingia uwanjani bure si jambo dogo. Nasi tunaahidi kushinda mchezo huo , tumejiandaa vyema kwa mchezo huu na kikosi tayari kinaendelea na mazoezi ," amesema Zoro.Afisa Habari wa Stand United FC, Ramadhani Zoro akizungumza na waandishi wa habari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com