
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abrahmani Abdallah, amewataka wanaTanga kutokubali kuingiliwa na watu kwa visingizio vya Siasa wakiwa na nia ya kuvuruga amani akisema kamwe jambo hilo CCM haitaweza kulivumilia.
Rajabu Abdarahman Abdallah amesema kwamba hata Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amejipambanua kwenye amani na yeyote atakayediriki kuchezea amani hatakuwa na mswalia
Mtume.
Mwenyekiti Rajabu Abrahmani Abdallah ameyasema hayo katika Salaam zake za Eid el Fitr kwa Waislamu wote na Wananchi wa Mkoa wa Tanga ikiwa zimesalia siku chache kukamilika kwa Ibada ya funga na kuingia kwenye kusherehekea Sikukuu hiyo ya Eid El Fitr.
Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Tanga alibainisha kuwa Serikali Mkoa wa Tanga ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Balozi Dkt. Batilda Salha Burian na kamati yake ya ulinzi na Usalama wamejiimarisha na kwamba anayetaka kuna aje kwa msingi wa utulivu.
Aidha amewasihi wananchi wote hususani waislamu kusherehekea Sikukuu ya Eid El fitri kwa amani na upendo huku akisema kuwa watakaoleta viashiria vya uvunifu wa amani wanapaswa kukemewa bila hofu.
Licha ya kutoa rai hiyo, Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa aliwashukuru Wananchi wa Mkoa wa Tanga katika kudumisha amani katika kipindi chote cha mwezi wa Ramadhani kipindi ambacho Ibada zilifanyika bila changamoto.
Kuhusu bei ya bidhaa katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Mwenyekiti Rajabu aliwapongeza wafanyabiashara kwa kuonesha ustaarabu wa kutopandisha bei kiholela.
Alisema kuwa bei za bidhaa zimekuwa za kawaida tofauti na vipindi vingine ambavyo baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wakigeuza mwezi wa Ramadhani kuwa ni kipindi cha 'kuchuma' wakilenga kupata faida kubwa.
"Tumewahi kushuhudia mwezi wa Ramadhani wa miaka iliyopita baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakigeuza kuwa mwezi huu ni wa kuchuma hivyo kupandisha bei ya bidhaa lakini kwa miaka takribani mitatu hii hawakufanya hivyo" alisema huku akiwapongeza wafanyabiashara.
Aidha Mwenyekiti Rajabu Abdarahman Abdallah amewasihi Wana Tanga kuendelea kusaidiana kama ambavyo walikuwa wakifanya katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani akiwasisitiza umuhimu wa kuonekana huruma.
Social Plugin