Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NANYUMBU AMCOS YANUNUA GARI LA MILIONI 185 KUBORESHA UKUSANYAJI WA MAZAO


Gari lililonunuliwa na Kikundi cha Nanyumbu AMCOS Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara
Collinis Nayakunga Naibu mrajis wa vyama vya Ushirika uthibiti kutoka Tume ya Maendeleo ya kilimo na Uchumi wa Tanzania akiwapongeza wana Chama cha Nanyumbu AMCOS Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara
Wanachama wa Nanyumbu AMCOS Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara wakiwa kwenye hafla hiyo ya kupokea gari hilo
Bakari Nakanga katibu wa Nanyumbu AMCOS Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara akizungumza na wanakikundi wa Nanyumbu AMCOS baada ya zoezi la kukabidhi wa gari kufanyika
Bi Grace Masambaji mrajis msaidizi mkoa wa Mtwara akizungumza na wanachama wa kikundi hicho cha Nanyumbu AMCOS Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara

***
Na Regina Ndumbaro-Nanyumbu-Mtwara.

Nanyumbu AMCOS, iliyopo wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara, imenunua gari lenye thamani ya shilingi milioni 185 kutokana na bei nzuri ya mazao ya korosho kwa msimu wa 2024. 

Katibu wa Nanyumbu AMCOS, Bw. Bakari Nakanga, amesema chama hicho chenye wanachama 468 kiliamua kununua gari hilo kwa mkopo kutoka Benki ya CRDB, tawi la Nanyumbu, ili kurahisisha ukusanyaji wa mazao kama korosho na ufuta.

Meneja wa Benki ya CRDB, Bw. James Kisumo, amethibitisha kuwa benki hiyo imewapatia mkopo Nanyumbu AMCOS kwa lengo la kusaidia uboreshaji wa shughuli zao za kilimo. 

Makabidhiano ya gari hilo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Uthibiti kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Ndg. Collinis Nayakunga, ambaye amewapongeza wanachama wa Nanyumbu AMCOS kwa hatua hiyo ya maendeleo.

Aidha, Ndg. Nayakunga amempongeza Bi. Grace Masambaji, Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Mtwara, kwa kusimamia vyama vya msingi kwa ufanisi pamoja na kushughulikia changamoto mbalimbali zinazojitokeza. 

Kwa upande wake, Grace Masambaji mrajis msaidizi mkoa wa Mtwara amemshukuru Ndg. Nayakunga kwa kutenga muda kutoka Dodoma kuja Mtwara kufuatilia maendeleo ya vyama vya ushirika, jambo ambalo limewafurahisha viongozi wa mkoa huo.

Mwenyekiti wa chama kikuu cha msingi kinachohudumia Mtwara, Namnyamba, Masasi na Nanyumbu (MAMCU), Alhaji Azam Mfaume maarufu kama Julajula, amewapongeza wanachama wa Nanyumbu AMCOS kwa kununua gari hilo na kuwasihi kulitunza ili liwasaidie kuongeza mapato.

 Pia, amewataka wanachama waendelee kushirikiana kwa karibu ili kubuni miradi zaidi ya maendeleo.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Ndg. Christopher Magala, ambaye alipewa jukumu la kukabidhi gari hilo rasmi kwa AMCOS.

 Amewataka viongozi wa Nanyumbu AMCOS kuendelea kubuni mbinu mpya za maendeleo ya kiuchumi. 

Kwa sasa, Nanyumbu AMCOS ina maghala matano ya kuhifadhia mazao, na meneja wa MAMCU tawi la Masasi, Ndg. Costa, amesifu hatua ya kununua gari aina ya Scania tani 20 kwa manufaa ya wanachama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com