Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC TANGA ATAKA VIONGOZI WA DINI KUIBEBA AGENDA YA UCHAGUZI MKUU

Na Hadija Bagasha Tanga, 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilida Buriani amewataka viongozi wa dini kuibeba agenda ya uchaguzi mkuu mwaka huu kwenye majukwaa yao na kuhakikisha viongozi wanaotaka kuingia madarakani kwa njia ya rushwa  Oktoba mwaka huu hawapenyi.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga ametoa kauli hiyo wakati akifungua semina kwa viongozi wa dini iliyoandaliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa Tanga ambapo  amewataka viongozi wa dini kutumia majukwaa yao kuielimisha jamii umuhimu wa kupambana na rushwa  na kushiriki kwa wingi kwenye kwenye zoezi hilo kwa lengo la kuwapata viongozi bora,.

Aidha Balozi Dkt Batilda Buriani amewataka viongozi wa dini Mkoani humo kutumia nafasi zao katika maeneo mbalimbali ikiwemo  nyumba za ibada kuendelea kukemea vitendo vya Rushwa  hususani kipindi hiki Taifa linapojiandaa kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais , Wabunge pamoja na Madiwani.

 Dkt  Batilda amesisitiza kuwa pamoja na dhamana waliyonayo kuwaongoza waumini kiimani wanawajibu pia wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupinga vitendo vya Rushwa ambavyo vimekuwa ni adui wa haki na Maendeleo kwa Taifa.

"Kama mnavyofahamu maadui wa kubwa wa maendeleo katika nchi yeyote ni Rushwa ambayo ni adui wa haki mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Rais , wabunge na Madiwani niwaombe sana viongozi wa dini  muendelee kuliombea Taifa amani Taifa  letu  lakini mkatoe elimu kwa waumini na wananchi kwa ujumla kuhusu kupinga na kukataa Rushwa hasa kipindi hiki". alisema Dkt. Buriani.

Kwa upande wake, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Ramadhan Ndwatah amesema taasisis hiyo imeamua kuwakutanisha viongozi hao kwa kutambua umuhimu wao kwa jamii. 

Kamanda huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga amebainisha kuwa kupitia uchaguzi wa wenyeviti wa Serikali za mitaa , vijiji na vitongoji  uliofanyika November 2024 walibaini baadhi ya vitendo vya Rushwa ambavyo walivichukulia hatua hivyo kuelekea uchaguzi mkuu viongozi wa dini wana nafasi kubwa kushiriki katika kampeni ya mapambano dhidi ya Rushwa.

"Tunashukuru kwamba uchaguzi wa wenyeviti wa Serikali za mitaa vijiji na vitongoji uliishia salama japo katika tafiti tulizozifanya  tulibaini baadhi ya vitendo vya Rushwa na wahusika walichukuliwa hatua , kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu viongozi wa dini kama wadau wetu wakubwa mama nafasi ya kushirikiana na sisi katika kampeni yetu ya kuzuia kupambana na vitendo vyote vya Rushwa" alisema Ndwatah. 

Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Tanga  Sheikh Juma Ruuchu ameishukuru na kupongeza taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa 'TAKUKURU' Mkoa wa Tanga kwa kuwapatia elimu hiyo viongozi wa dini akiwataka kwenda kupelekea ujumbe huo kwa wananchi..

"Tunawashukuru na kuwapongeza sana wenzetu wa TAKUKURU kwa kuona na kutambua nafasi yetu katika jambo hili ambalo bado linaleta shida katika nchi yetu na sisi tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwao na kwenda kupeleka ujumbe wa elimu hii kwa waumini na wananchi wote tunaowaongoza", alisema Sheikh.

Baadhi ya viongozi wa dini waliohuduruia kikao hicho wameahidi kuyatumia majukwaa yao  ya kidini kutoa elimu ya mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa  kwenye uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.

Elimu hiyo inalenga kuifanya jamii kuchagua viongozi bila kuwepo kwa misingi ya rushwa ikiaminika kuwa  viongozi watakaopatikana na kwa njia hiyo ni wale ambao watakuwa wakitanguliza maslahi yao mbele  na kujinufaisha  kiuchumi huku wakijitahidi  kurejesha fedha na mali walizozitumia kwenye uchaguzi huo kuwarubuni wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com