
Na Hadija Bagasha - Tanga
Halima Mohamed ni mlemavu wa viungo ambaye anatumia kiti mwendo kufanya shughuli zake kiuchumi mbali na ulemavu alionao anajishughulisha na ufundi cherehani kazi ambayo ameianza toka akiwa na miaka 14.
Ndoto yake ilikuwa ni kumiliki mashine ya kushoenea nguo yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha kiwango anachokihitaji kwajili ya kukidhi mahitaji ya maisha yake lakini pia na familia yao.
March 30 mwaka huu ndoto ya Halima inaanza kutimia pale ambapo anakabidhiwa mashine ya cherehani kutoka kwa kikundi cha wakinamama dhehebu la bohora ambao katika pitapita zao walikuwa wakitafuta mtu mwenye mahitaji ambaye watamuwezesha kama sehemu ys kumjengea uwezo wa kufikia malengo yake.
Halima amesema msaada huo kwake umekuja kwa wakati muafaka na kwamba hata kiwango cha nguo alichokuwa akishona kitaongezeka mara dufu na hivyo kuwashukuru kwa namna ambavyo waliona yeye ni mtu mwenye uhitaji.
Wakati Wanawake hao wakitoa msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Salha Burian naye ameahidi kukabidhi mashine nyingine mbili kwa lengo la kuiinua jamii hiyo.
Aidha kikundi hicho cha Wanawake wa madhehebu ya Bohora cha Jijini Tanga wamekabidhi mashine mbili (2) za cherahani kwa jamii ya watu wenye mahitaji maalum lengo likiwa kuwawezesha kiuchumi.
Gharama halisi ya mashine hizo 'cherahani moja imeelezwa kuwa Shilingi 700,000/- na hivyo dhehebu hilo la Bohora limegharimia jumla ya Shilingi 1,400,000/- mil.
Wakati Wanawake hao wakitoa msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Salha Burian naye ameahidi kukabidhi mashine nyingine mbili kwa lengo la kuiinua jamii hiyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Salha Burian alisema,atahakikisha kunapatikana jengo maalum ili kiwakusanya Wanawake hao wenye mahitaji maalum ambapo watapata eneo kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.
"Kuna majengo yapo maeneo jirani tutaangalia namna ya kupata mojawapo ili kiwakusanya ndugu zetu hawa,wataendeshea shughuli zao hapo huku tukiwasaidia kupata wateja"alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Social Plugin