Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AKIPIKA NYAMA,WALI, AKABIDHI ZAWADI ZA RAIS SAMIA KWA WATOTO KAHAMA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA EID AL - FITR


Na. Paul Kasembo, KAHAMA MC.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametoa mkono wa Eid Al - Fitr kwa Makao ya Watoto Yatima katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na Kishapu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu hii pamoja nao kupitia zawadi hizo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, RC Macha alisema kuwa wao kama wasaidizi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wameagizwa kupeleka zawadi hizo kwa watoto hao ili kuwashika mkono katika kusherehekea Sikukuu hii na kwamba anatambua uwepo, anathamni, anaheshimu na anawajali sana wao kama sehemu ya jamii na kwamba wao pia kama walivyo watoto wengine wanazo haki na stahiki sawa sawa.


"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuagiza tuje kuwaletea zawadi hizi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu hii ya Eid Al - Fitr pamoja naye ambapo ametupatia vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Mafuta ya Kupikia, mboga (mbuzi), Sharubati (juice), maji, sabuni na maziwa kwa watoto wachanga hivi vyote ametoa tuwaletee na ametoa salamu zake kwenu kuwa anawapenda sana," alisema RC Macha.


Awali akitoa salamu za utangulizi kwa watoto hao katika nyakati tofauti, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita  aliwaeleza watoto hao kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Kiongozi wa Nchi na Mama wa Watoto wote na ndiyo sababu leo tumekuja na Mhe. RC Macha kuwaletea zawadi hizi maalum kwa siku ya leo na kila mtoto atafurahia naye kwa kuwa kwake watoto wote ni sawa.


Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi mbalimbali kwenye Makao ya Watoto Yatima 6 na Makazi ya Wazee Wenye Mahitaji Maalum 1 ambapo sehemu zote hizo wamepatiwa mchele, mafuta ya kupikia, mboga (mbuzi), sukari, Sharubati (juice), maji, sabuni na maziwa kwa watoto wachanga huku RC Macha pamoja na pongezi kwa wamiliki wa Makazi na Makao lakini pia amekiri kupokea changamoto walizonazo Wamiliki, Walezi na Waanzilishi wa Makao na Malezi na anakwenda kuzifanyia kazi.


Utekelezaji huu wa kutoa zawadi na kushiriki furaha ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kusherehekea Sikukuu hii ya Eid Al - Fitr ni wa kila mara kwani anatambua, anathamini, anaheshimu uwepo wao kama sehemu ya jamii yake na kwamba anawapenda sana na ndiyo sababu kila wakati anawafikia na kuwapa tabasamu kupitia Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya mkoani Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com