Na Hamida Kamchalla, TANGA.
SHIRIKA la Jhpiego kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na TAMISEMI limejikita kushirikiana katika afua ya kuzuia saratani ya matiti itakayo tekelezwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu.
Mkurugenzi wa mradi wa Pfizer Breast Cancer Dkt. Maryrose Gattas ametasema hayo leo Kwa mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batilda Buriani na kubainisha kwamba mradi huo unatekelezwa katika awamu mbili na unafadhiliwa na The Pfizer Foundation.
Amesema mradi huo, kwa awamu ya kwanza tayari umetekelezwa kuanzia Januari hadi Desemba, 2024 ambapo awamu ya pili utatekelezwa kwa miaka mitatu, kuanzia mwaka 2025/27.
"Katika awamu ya kwanza tumetekeleza mradi huu katika Mikoa miwili kwa Bara ambayo ni Tanga na Mwanza, wakati Zanzibar umetekelezwa katika Mkoa wa Pemba, na tulijikita katika kuelimisha jamii kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kufanya uchunguzi wa awali,
"Maambukizi ya saratani ya matiti yanaweza kumpata yeyote awe mwanaume au manamke, lakini kwa wanawake wana asilimia 100 kupata maambukizi zaidi ya wanaume", amesema Dkt.
Lakini pia Dkt. amesema mradi huo umewajengea uwezo wahudumu wa afya kuanzia ngazi ya halmashauri, hadi Mkoa, vikiwemo vituo vya kutolea huduma hiyo na kwamba katika awamu ya kwanza mafanikio ni mazuri.
Amebainisha kwamba katika awamu ya pili ya mradi huo Shirika litajikita katika mkakati ile ile ya utekelezaji wa awamu ya kwanza, na hiyo ni baada ya ufanisi mzuri uliofanyika.
"Tutaboresha kuhakikisha kwamba wananchi wanafahamu jinsi ya kujipima saratani ya matiti pamoja na kuwawezesha watoa huduma za Afya kutumia utaalamu na vigezo ambavyo vimewekwa Kitaifa", amefafanua.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batilda Buriani amesema kwakuwa mradi huo unakwenda miaka mitatu wataalamu wa afya hawana budi kujipanga kuhakikisha unaendeleaje.
"Wataalamu wa afya wazingatie maadili ya taaluma zao na kufanya kazi kwa weledi ili kufanikisha mradi huu kutekelezwa kwa ufanisi na kupata matokeo mazuri zaidi", amesema.
Social Plugin