NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Posta Tanzania limeingia makubaliano ya ushiriano na Bahati Nasibu ya Tanzania ili kuongeza upatikanaji wa michezo ya kubahatisha nchini.
Kwa kutumia miundombinu madhubuti ya Shirika la Posta Tanzania, Jukwaa la Bahati Nasibu ya Taifa linalenga kutoa michezo iliyo rafiki, rahisi na yenye uwazi kwa washiriki wote, ikiimarisha dhamira yake ya kuboresha maisha ya watanzania kote nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo leo Machi 20, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara za Kielektroniki na Huduma za Kifedha wa Shirika la Posta Tanzania, Constantine Kasese amesema kupitia upatikanaji wa majukwaa ya bahati nasibu katika ofisi zao, itasaidia kuleta urahisi wa upatikanaji wa tiketi za michezo ya kubahatisha na kuchangia juhudi za taifa za kuwainua wananchi.
" Tumejikita katika kuwaunganisha watu na huduma muhimu kote nchini. Ushirikiano huu unawiana na maono yetu ya kutoa huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu". Amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ithuba Tanzania, Kelvin Koka amesema dhamira yao ni kuhakikisha kila mtanzania anaweza kushiriki katika michezo ya kubahatisha.
Social Plugin