
*****
TAMASHA la kuombea Uchaguzi
Mkuu kufanyika mikoa 26 kuanzia jijini Dar es Salaam mwaka huu ambapo waimbaji mbalimbali
wanatarajiwa kupamba tamasha hilo.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Machi 24, 2025, Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amesema
kuwa ibada hiyo itakuwa ni ya Maandalizi ya kuelekea Uchaguzi.
"Lengo ni kuweka umoja
na ushirikiano watanzania kuombea uchaguzi kufanyika kwa Amani na kupata
viongozi ambao watatuongoza kwa hekima na busara.
"Waimbaji kutoka
Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda wanatarajia kupamba tamasha hilo la uimbaji
na Maombi ya uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Aidha ameongeza kwa
kuwaomba viongozi wa vyama vya siasa kutumia lugha zisizo za matusi katika
mikutano yao bali kutumia lugha za siasa zenye heshima hata kwa vizazi vyetu.
Pia amewaomba wadau na watu
mbalimbali kujitokeza kutoa ushirikiano wa kudhamini ili kufanikisha tamasha
hilo
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin