Habari Mpya

    Loading......

TRA KUENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WATUMISHI WAKE WANAOENDA KINYUME




Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA )
imewachukulia hatua baadhi ya watumishi wanaoenda kinyume na maadili kwa kuwafukuza kazi watumishi 14,kuwashusha mishahara watumishi 6,kuwashusha cheo na kuwapunguzia mishahara watumishi 6 na kuwapa onyo la maandishi watumishi 22.

Kamishina Mkuu wa mamlaka hiyo Yusuphu Juma Mwenda ameeleza hayo leo March 12,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo na kuwataka wafanyabiashara, wadau na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa wakati na hiari kuepukana na riba.

Kamishina Mwenda amewahakikishia watanzania yakuwa mamlaka hiyo itaendelea kutekeleza maagizo Mhe.Rais yakuwa na mfumo wa kodi unaotabirika,wenye usawa,unaotenda haki kwa kila mmoja na unaowezesha kukua kwa biashara sambamba na kuendelea kuimarisha ushirikiano na viongozi wa wafanyabiashara.

"Hakuna anayeweza kukusaidia kutokulipa kodi halalii: Atakusaidia kuihairisha, lakini itakuja kujulikana na utalipa pamoja na riba na adhabuTunawahakikishia kuendelea kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais ya kuwa na mfumo wa kodi unaotabirika, wenye usawa, unaotenda haki kwa kila mmoja pamoja na unaowezesha kukua kwa biashara. 

Aidha, tutaendelea kuimarisha ushirikiano na viongozi wa wafanyabiashara, wafanyabiashara wenyewe pamoja na makundi mbalimbali ndani ya jamii",amesema.

Pia amewakumbusha wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa Risiti za kielektroniki (EFD)kila wanapouza bidhaa na huduma mbalimbali na kuwasilisha ritani za kila mwezi na Kuhakikisha hawajiingizi katika ununuzi wa risiti za EFD bandia .

Aidha amesema miongoni mwa mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita nipamoja na Kuimarisha Weledi na Uadilifu wa Watumishi wa mamlaka hiyo na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria kwa wachache wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma .

Amesema "Mafanikio ndani ya miaka minne yaliyotokana na utekelezaji wa Maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia, Suluhu Hassan:Kusimamia uadilifu kwa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria kwa wachache wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa watumishi wote wa TRA unaotokana na weledi na uwajibikaji uliosisitizwa na Mheshimiwa Rais.

"TRA katika kipindi cha miaka minne, imechukua hatua zifuatazo kwa wachache wanaoenda kinyume na maadili 1. Kufukuzwa kazi -14,2. Kushushwa Mshahara- 6,3. Kushushwa cheo na kupunguzwa mshahara- 12,4. Kupewa Onyo la Maandishi - 22",amesema.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com