Habari Mpya

    Loading......

TUSIWACHAGUE WAONGO WATAKWAMISHA MAENDELEO: FARIS BURUHAN


Na Lydia Lugakila -Ngara

Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Kagera Faris Buruhan amewataka wananchi katika wilaya ya Ngara Mkoani Kagera kutowachagua viongozi waongo ambao hawawezi kuleta maendeleo katika jamii.


Faris ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Jumuiya ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari ya Omurusagamba iliyopo katika kata ya Omurusagamba wilayani Ngara Mkoani Kagera.


Faris amewaeleza Wanafunzi hao malengo ya kufika katika shule hiyo kuwa ni kwa ajili ya kufanya kampeini maalum ya kutafuta kura za Dkt. Samia Suluhu Hassan na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Taifa ambaye aliteuliwa na Wajumbe wa halmashauri kuu kuwa mgombea Urais Kupitia chama cha Mapinduzi.


Faris amewaambia wanafunzi wa shule hiyo ambao wametimiza miaka kumi na nane kufanya mchakato wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kupata haki ya kupiga kura na kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwachagua wabunge na madiwani watakaoletwa na chama hicho.


"Waongo ni waongo tu hawatakiwi kuchaguliwa na kupewa kura maana hawana nafasi yoyote ya kuleta maendeleo katika Nchi na jamii kwa ujumla kwa kuwa wamekuwa wakidai katiba mpya ambayo haiwezi kuwasiadia chochote katika nchi hii",amesema.


Hata hivyo baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha tano na sita kutoka shule ya sekondari a Omurusagamba wamesema kuwa wao wapo tayari kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura ili waweze kumpigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya mambo makubwa katika nchi hii kwa kuboresha miundombinu ikiwemo elimu Afya ujenzi wa mabweni pamoja na huduma nyingine za maendeleo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com