Na Hadija Bagasha Tanga,
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (UWASA) inatarajia kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 45 hadi lita milioni 60 ifikapo Desemba mwaka huu, baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa hati fungani unaogharimu zaidi ya bilioni 53.
Mradi huo utahakikisha miji ya Tanga, Pangani na Muheza inapata huduma ya maji kwa asilimia 100.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Tanga UWASA, Alawi Ahmad, alitoa taarifa hiyo katika mkutano wa waandishi wa habari March 17 mwaka huu kuelekea maadhimisho ya Wiki ya Maji.
Alisema kwamba uzalishaji wa maji utaongezeka kwa asilimia 25, kutoka lita milioni 45 hadi lita milioni 60.
Aliongeza kuwa mtandao wa mabomba utaongezwa kwa kilomita 60 ili kufikia maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo, hivyo kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa idadi ya watu wote.
Mradi huo ulianza Agosti mwaka jana na unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu Hadi sasa, umefikia asilimia 15, ambapo vifaa vyote vimeshawasili na wakandarasi wameanza kazi katika maeneo mbalimbali.
Kaimu Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Salum Hamisi, alisema mradi huu unalenga kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa Tanga, Muheza na Pangani. Alifafanua kuwa mtambo wa Mabayani utapanuliwa ili kuongeza uwezo wake kutoka lita milionini 45,000 hadi lita milioni 60,000 kwa siku.
Aidha, mradi huu utajenga bomba kubwa kutoka Mabayani hadi Mowe na kuongeza uwezo wa kituo cha kusafisha maji cha Mowe. Vilevile, tenki kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 35,000 litajengwa ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wananchi hata wakati wa changamoto za upungufu wa maji.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (UWASA) imekuwa ikifanya juhudi za kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi katika miji ya Tanga, Pangani, na Muheza,zalishaji wa maji umekuwa ni changamoto kutokana na ongezeko la idadi ya watu na hali ya mabadiliko ya tabia nchi.
Social Plugin