Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UWT WALAANI SHAMBULIO LA MWENEZI BAWACHA



Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) umelaani vikali chambulio la Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) Siglada Mligo (34)lililotokea tarehe 25 machi,2025 Mkoani Njombe.

Taarifa zinaeleza kuwa Mwenezi huyo alipigwa na walinzi wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche usiku wa juzi(March 25, 2025)mkoani Njombe, katika kikao cha ndani cha chama hicho.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo machi 28 mwaka huu Jijini Dodoma katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Dodoma Mwenyekiti wa UWT Mary Chatanda amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kumsaka mtuhumiwa na kumfikisha katika vyombo vya sheria kwakuwa wapo tayari kutoa msaada wa kisheria kwa kutoa mwanasheria ili haki iweze kupatikana kwa mhanga wa tukio hilo.

"Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kuendelea kumsaka mtuhumiwa na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria,UWT ipo tayari kumuwekea mwanasheria ili haki iweze kupatikana." Amesema Chatanda

Chatanda amesema anashangazwa na ukimya wa viongozi wa Baraza la Umoja wa Wanawake wa Chadema juu ya shambulio la kudhuru mwili kwa kiongozi wa ngazi ya juu wa baraza hilo kwa nafasi ya mwenezi.

"Kutokemea matumizi ya nguvu kwenye tofauti ya kisiasa ndani ya chama hiko ni dalili ya uoga dhidi ya mfumo dume wa chama cha Chadema.

Aidha ameiomba ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kufuatilia kwa karibu uanzishwaji wa madawati ya jinsia kwa vyama vya siasa na kuangalia utekelezaji wa majukumu yake ili madawati hayo yawe na uwezo .

"Tunataka mamlaka ichukue hatua dhidi ya vitendo vya unyanyasaji na ukandamizaji dhidi ya wanawake kwakuwa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2023 imevitaka vyama vya siasa kuanzisha madawati hayo," ameeleza.

Mwenyekiti huyo pia ametumia nafasi hiyo kuhamasisha wanawake kujiandaa na kujitokeza muda ukifika wa kuchukua fomu za nafasi ya ubunge wa majimbo na udiwani wa kata ndani ya vyama mbali mbali kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025.

Kutokana na tukio hilo baadhi ya wadau wa siasa mkoani Njombe ambao walishuhudia tukio hilo wameeleza kuwa vurugu hizo zilitokea baada ya mabishano makali kuhusu masuala ya uongozi na mwelekeo wa chama, ambapo Siglad alionekana kutofautiana na mtazamo wa kundi linalomuunga mkono Heche.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hii shuhuda huyo ameeleza kuwa Walinzi wa Heche walidaiwa kumpiga kwa nguvu na kumdhalilisha, hali iliyosababisha taharuki miongoni mwa wanachama waliokuwepo.

"Huu ni udhalilishaji na ukiakwaji wa haki za wanawake, tukio hilo linaleta picha ya mpasuko unaozidi kujitokeza ndani ya CHADEMA, hasa kati ya viongozi wanao unga mkono kususia uchaguzi na wasio unga mkono kususia uchaguzi,mgawanyiko huu unaonekana kuchochewa na siasa za makundi ndani ya chama hicho,lazima hatua stahiki zichukuliwe mapema kuepusha madhara mengine, "ameeleza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com