Na Elizabeth John, NJOMBE.
WANANCHI mkoani Njombe wameitwa kwenye viwanja vya Sabasaba mjini humo ili kujifunza fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye mazao ya misitu ikiwemo mbao na nguzo.
Wito huo umetolewa leo na Ofisa Habari na Mawasilino kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ridhiwani Gambalela mjini Njombe kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Misitu Duniani kitaifa mkoani humo.
Amesema elimu hiyo itamsaidia mwananchi kujua namna gani anaweza kujiingiza kwenye fursa hizo kupitia wataalamu waliopo sambamba na kujua namna bora ya ufugaji wa nyuki.
Social Plugin