Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA ZA ROBO YA TATU MWAKA WA FEDHA 2024/2025

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Willium Jijimya akizungumza Leo Aprili 29,2025 kwenye kikao cha baraza la madiwani la kupokea na kujadili taarifa za Kata robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025 lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akifuatilia kikao cha baraza la madiwani cha kupokea taarifa za Kata robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika Aprili 29,2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

****

Na Sumai Salum-Kishapu 

Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga limepokea na kujadili taarifa za Kata zake ishirini na tisa robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2024/2025

Akizungumza kwenye baraza hilo lililofanyika Aprili 29,2025 katika ukumbi wa Halmashauri mwenyekiti wa Halamashauri Mhe.Willium Jijimya amempongeza Mkurugenzi mtendaji Emmanuel Johnson na wasidizi wake kwa utendaji kazi mzuri huku akiwasihi kuongeza bidii ya kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com