Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dokta. Doto Biteko leo Aprili 16,2025 ameongoza maelfu ya waombolezaji pamoja na viongozi mbalimbali kwenye shughuli ya maziko ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga .
Mazishi ya Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga yamefanyika katika eneo la Migungani Wilayani Bunda Mkoani Mara.
Akizungumza mara baada ya ibada ya mazishi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Biteko amemuelezea marehemu Mhandisi Gissima kuwa ameacha urithi mkubwa wa muunganiko ndani ya TANESCO wenye lengo la kuhakikisha Watanzania wanapata umeme wakati wote.
Dkt. Biteko amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alimuamini kutokana na uwajibikaji wake hivyo ametuma salamu za pole kwa familia, Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO ambapo amefafanua kuwa ameacha alama kubwa hasa katika kuhakikisha miradi ya umeme inakamilika kwa wakati na Watanzania wananufaika na nishati hiyo muhimu.


“Nitoe pole sana kwa familia kwa kuwa imepata pigo lakini kutokana na mema aliyoyafanya wakati wa uhai wake ni faraja kubwa.Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuona marehemu Mha. Gissima anafaa ndani ya Shirika na hakika kazi yake ya kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika imeonekana’’Aliongeza Dkt Nyansaho.
Social Plugin