
Na Mwandishi wetu- Malunde 1 blog
Diwani wa Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Gulamhafeez Mukadam, ameendelea kuonesha dhamira yake ya kuboresha sekta ya elimu kwa vitendo, baada ya kufanya ziara ya kutembelea shule na vyuo mbalimbali vilivyopo ndani ya kata ya Mjini huku akikabidhi vifaa mbalimbali vya kusaidia maendeleo ya wanafunzi.
Ziara hiyo imefanyika leo Aprili 09, 2025 kutembelea katika shule za Town Sekondari, Uhuru Sekondari, Buluba sekondari, Town Shule ya Msingi, Mwenge Shule ya Msingi, pamoja na vyuo viwili ambavyo ni Chuo cha Maendeleo ya Jamii Hombolo tawi la Shinyanga na Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) huku akiongozana na kamati ya siasa ya kata ya Mjini.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mukadam amesema kuwa lengo la ziara ni kujionea hali ya mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi, kuwasikiliza walimu na wanafunzi, pamoja na kutimiza ahadi alizotoa awali ikiwemo kusaidia ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya sekondari Town ambapo ameweza kuchangia masinki 9 pamoja na fedha shilingi 100,000/= ili kusaidia ujenzi wa vyoo kwaajili ya wanafunzi na waalimu.
“Dhamira ya ziara yetu siku ya leo ni kutimiza ahadi yangu niliyoitoa kwenye shule za msingi na sekondari ndani ya kata ya mjini ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa kwa ajili ya michezo ambapo leo tunakabidhi mipira pamoja na jezi kwaajili ya michezo lakini pia mashine za kushonea nguo (cherehani) ili ziweze kuwasaidia shuleni kama mradi shuleni pamoja na kujifunza ushonaji kwa vitendo, gharama za vifaa hivi ni shilingi Milioni 4.5 ikijumuisha vifaa vya michezo na cherehani”, amesema Mhe. Gulamhafeez.
Aidha amewaomba wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi CCM ambacho kimeleta maendeleo katika sekta mbalimbali.
Baadhi ya walimu na wanafunzi waliopokea vifaa hivyo wameeleza furaha na kutoa shukrani kwa Mhe. Gulamhafeez kwa kutimiza ahadi zake na kuonesha moyo wa kujali maendeleo ya elimu pamoja na vipaji vya wanafunzi shuleni.
“Tunamshukuru sana Mhe. Diwani kwa kuipa kipaumbele sekta ya elimu, vifaa hivi vitatusaidia sana kwenye michezo. Mashine za kushona zitawasaidia wanafunzi wetu kujifunza stadi za maisha lakini pia kutengeneza sare za wanafunzi kwa gharama nafuu”, amesema Mwl. Victoria Nakiliaumi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Uhuru
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akikabidhi jezi na mipira kwa wanafunzi Shule ya Sekondari Town.
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akikabidhi jezi na mipira kwa wanafunzi Shule ya Sekondari Town.
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akikabidhi cherehani kwa mkuu wa Shule ya Sekondari Town pamoja na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo..
Cherehani iliyotolewa na Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam.
Katibu wa CCM kata ya Mjini Rashid Abdullah akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Baadhi ya wanafunzi shule ya Msingi Town.
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akikabidhi jezi, mipira na cherehani kwa mwalimu wa shulke ya msingi Town.
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akizungumza na wanafunzi katika shule ya msingi Mwenge mara baada ya kukabishi vifaa hivyo.

Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam pamoja na kamati ya siasa kata ya Mjini wakikabidhi cherehani kwa waalimu na wanafunzi wa shule ya awali na msingi Mwenge.
Baadhi ya wanachuo wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Hombolo tawi la Shinyanga.
Baadhi ya wanachuo wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Hombolo tawi la Shinyanga.
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo katika shule ya sekondari Buluba.
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akikabidhi jezi na mipira kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Buluba.
Mkuu wa shule ya Sekondari Buluba Kisaku William akitoa shukurani za dhati mara baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka kwa
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam.
Mkuu wa shule ya sekondari Uhuru Mwl. Victoria Nakiliaumi akizungumza mara baada ya kukabishiwa vifaa hiyo.

Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akizungmza na wanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru.
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akikabidhi kwa wanafunzi vifaa vya michezo shule ya sekondari Uhuru.
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akikabidhi cherehani kwa Mkuu wa shule ya sekondari Uhuru Mwl. Victoria Nakiliaumi.
Diwani wa Kata ya Mjini, Mhe. Gulamhafeez Mukadam akikabidhi jezi na mipira kwa Mratibu wa michezo chuo cha SHYCOM Mwl. Shinje Martine.

Social Plugin