Mashabiki wa muziki wa asili mpo? 🎶
Msanii mahiri wa muziki wa Kisukuma, Ng'wana Kang'wa, amefungua rasmi mwaka 2025 kwa albamu yake mpya iitwayo “MBINA” – yenye jumla ya ngoma tisa kali, zenye ujumbe mzito, midundo ya asili na roho halisi ya utamaduni wetu! 🇹🇿
Albamu hii ni kama safari ya maisha halisi—kuanzia mapenzi, harusi, elimu, haki, changamoto hadi kuenzi mila zetu—yote yamefungwa katika ngoma zenye burudani na mafunzo.
🎧 Zisikilize Hapa Ngoma Zote 9 Kutoka “MBINA”👇
-
🔥 PESA
Fedha inavyobadili mitazamo na maisha ya watu – Ng'wana Kang'wa anaichambua kwa ustadi.
-
🔥 NALHI NANI?
Tafakari juu ya utambulisho binafsi – “Mimi ni nani?”
-
🔥 WAKUSOMA
Mtoto wa kike mwanafunzi aliyekengeuka – ujumbe wenye nguvu na uhalisia wa kijamii.
-
🔥 HAKI SAWA
Haki na usawa wa kijinsia – sauti ya wanaume pia imesikika hapa.
-
🔥 MISHINGA
Ngoma kali ya utamaduni – Kang'wa anadhihirisha uwezo wake katika nyanja zote.
-
🔥 MBINA
Wimbo wa jina la albamu – maisha ya kijijini, mshikamano na utu.
-
🔥 SUMU KALI
Onyo kali kuhusu tabia mbaya za baadhi ya watu – usikubali kuyumbishwa!
-
🔥 MOYO
Mapenzi ya kweli – wimbo wa kugusa hisia hadi moyoni kabisa.
-
🔥 MILA
Heshima kwa mila na tamaduni za Kisukuma – urithi wa kitamaduni kwa sauti ya sasa.

📌 Albamu nzima inapatikana kwenye kituo rasmi cha YouTube cha Ng'wana Kang'wa:
👉 @ngwanakangwa na Malunde.com au Ng'wana Kang'wa - Malunde 1 blog
🛑 Usikubali kupitwa! Hizi ni ngoma zenye ladha ya jadi, busara na burudani ya hali ya juu.
🎤 Sikiliza, share na support muziki wa asili ya Tanzania! 🔥
Ng'wana Kang'wa - Pesa
Ng'wana Kang'wa - Mila

Ng'wana Kang'wa ni Msanii wa nyimbo za asili zenye mahadhi ya asili ya Afrika kupitia Kundi la BTM Africa, anayepatikana Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga anasifika kwa kuchanganya muziki wa asili na vipengele vya kisasa, akitumia ala za jadi kama ngoma na filimbi, pamoja na sauti za kisasa kama gitari na keyboard.
Social Plugin