Mwenyekiti wa Misa-Tanzania Edwin Soko (kushoto)akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Nchini Tanzania Michel Toto.
Na Marco Maduhu,ARUSHA
BAADHI ya Wanachama wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA TAN) Tawi la Tanzania, wamekutana na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Nchini Tanzania Michel Toto, katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kuendeleza majadiliano kuhusu hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wa habari na mashirika ya kimataifa kama UNESCO.
Katika majadiliano yao, wamegusia changamoto zinazoikumba sekta ya habari, ikiwemo mazingira ya kazi kwa wanahabari, pia umuhimu wa kuwalinda wanahabari na kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uhuru na usalama.
Aidha, wametafakari pia fursa zilizopo kwa maendeleo ya tasnia ya habari kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa, mafunzo endelevu kwa wanahabari, pamoja na uimarishaji wa misingi ya maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Ushirikiano na mashirika kama UNESCO umetajwa kuwa nguzo muhimu katika kufanikisha malengo hayo ya Tasnia ya Habari.
Social Plugin