
Taarifa hii imetolewa rasmi na Mwenyekiti wa SHYTOWN ViP, Ndugu Musa Ngangalas, kufuatia kikao cha mwaka cha wanachama kilichofanyika tarehe 6 Aprili 2025.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Ngangalas, sherehe ya mwaka huu inatarajiwa kuwa ya kipekee, ikiwa imeandaliwa kwa kiwango cha juu ili kuwapa wanachama wote nafasi ya kufurahia, kujifunza, na kubadilishana mawazo ya maendeleo.
“Tunaamini kwamba kupitia mkusanyiko huu wa wanachama, tutaendelea kudumisha mshikamano na kuongeza nguvu ya pamoja katika kufikia malengo ya SHYTOWN ViP,” amesema Musa Ngangalas.
SHYTOWN ViP imekuwa na utaratibu wa kuandaa sherehe ya mwaka kwa ajili ya kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano baina ya wanachama wake.
Sherehe hizi pia hutoa fursa ya kupitia mafanikio yaliyopatikana kwa mwaka mzima na kuweka mikakati ya maendeleo kwa mwaka unaofuata.
Wanachama wote pamoja na wale wanaotamani kuwa sehemu ya SHYTOWN ViP wanakaribishwa kuhudhuria sherehe hii muhimu.
Maelezo ya mahali itakapofanyika na ratiba ya siku hiyo yatatolewa hivi karibuni kupitia njia rasmi za mawasiliano ya kikundi.
Social Plugin