Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA 'SPC' YAFANYA MKUTANO MKUU, MAHAKAMA KUU YATOA NENO

 
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imeahidi kushirikiana kwa karibu na vyombo vya habari mkoani humo kwa kuanzisha mafunzo maalum ya uandishi wa habari za kimahakama, huku ikiwataka waandishi kuhakikisha wanazingatia maadili, sheria na vyanzo sahihi hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu.

Ahadi hiyo imetolewa na Jaji Ntuli Mwakahesya alipomwakilisha Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali, katika Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club -SPC) uliofanyika leo Jumamosi Aprili 5,2025 kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Shinyanga Ntuli Mwakahesya.

“Mahakama iko tayari kutoa mafunzo kwa waandishi ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi kuhusu shughuli za kimahakama. Vyombo vya habari ni daraja muhimu kati ya Mahakama na wananchi,” amesema Jaji Mwakahesya.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa SPC, Greyson Kakuru, amesisitiza kuwa bado kuna changamoto kwa wanahabari wengi katika kuandika habari za kimahakama na uchaguzi kwa usahihi, hivyo ushirikiano huo utawasaidia kuongeza weledi na uelewa wa sheria.

SPC Yajivunia Mafanikio ya Miaka 5

Katika mkutano huo, SPC imeainisha mafanikio kadhaa yaliyopatikana kati ya mwaka 2020 hadi 2025, ikiwa ni pamoja na kuendesha kampeni dhidi ya ukatili ya Tsh milioni 66.7, kufungua ofisi ya waandishi wa habari wilayani Kahama, Kuongeza wanachama, rasilimali na ushawishi kitaifa, Kutangazwa na SIDA kama Klabu Imara na Bora, kutoa mafunzo na ziara za kitaaluma kwa wanachama na kukuza sauti za jamii kupitia redio na miradi ya habari.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru.

Kakuru amesema mafanikio hayo ni matokeo ya mshikamano miongoni mwa wanachama, Kamati Tendaji na Sekretarieti ya SPC.
Shukrani na Wito kwa Wadau

SPC imetumia jukwaa hilo kutoa shukrani kwa taasisi mbalimbali zilizochangia mafanikio ya klabu hiyo ikiwemo Mahakama Kuu, TASAF, CRDB, RUWASA, SHIDEFA, Life Water International, Kampuni ya Jambo Group, Jeshi la Zimamoto na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga huku ikikaribisha wadau wengine.

Aidha, imetoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kushirikiana na klabu hiyo katika kuendeleza tasnia ya habari na kuimarisha utoaji wa taarifa sahihi kwa jamii.

Katika mkutano huo, masuala ya uendeshaji wa klabu, tathmini ya mwaka uliopita na mipango ya maendeleo ya mwaka huu yanajadiliwa kwa kina lengo likiwa ni kuimarisha mshikamano na malengo ya kulinda maslahi ya wanahabari mkoani Shinyanga.


Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Shinyanga Ntuli Mwakahesya akizungumza kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali kwenye  Mkutano Mkuu wa SPC. Picha na Marco Maduhu na Kadama Malunde
Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Shinyanga Ntuli Mwakahesya akizungumza kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali kwenye  Mkutano Mkuu wa SPC.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Habari na Mawasiliano kutoka TASAF Christopher Kidanka akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Habari na Mawasiliano kutoka TASAF Christopher Kidanka akizungumza kwenye mkutano huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com