Na Sumai Salum - Kishapu
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga kupitia Jumuiya ya Wazazi, kimezindua rasmi Wiki ya Wazazi kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika Wilaya ya Kishapu, ikiwemo ukaguzi wa miradi ya maendeleo, upandaji miti na mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Bunambiyu.
Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 9, 2025, ukihudhuriwa na viongozi wa chama, jumuiya zake, wanachama pamoja na wananchi, ambapo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, alikuwa mgeni rasmi.
Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara, Mhe. Mlolwa amewahimiza wazazi kushiriki kikamilifu katika malezi bora ya watoto na kusimamia maadili ya jamii, akieleza kuwa wazazi ni nguzo muhimu ya kuimarisha msingi wa taifa.
Aidha, ametumia jukwaa hilo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayogusa sekta mbalimbali mkoani Shinyanga, ikiwemo elimu, afya na miundombinu.
Katika ziara hiyo, Mlolwa ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika shule ya sekondari Bunambiyu ambapo Mkuu wa shule hiyo, Mzee Matata Joel, ameeleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 166.4 zimetolewa na serikali ndani ya miaka mitano, fedha ambazo zimetumika kujenga madarasa, ofisi za walimu na matundu ya vyoo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga, John Siagi, amesema kuwa wameandaa mpango kazi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa CCM.
Ametumia nafasi hiyo pia kuhimiza wazazi kutoa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, pamoja na kuhakikisha malezi bora kwa vijana.
Maadhimisho hayo yamehusisha pia zoezi la upandaji miti katika eneo la shule ya Bunambiyu, kama ishara ya utunzaji wa mazingira na kuhimiza jamii kushiriki katika shughuli za kijani.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga leo Aprili 9, 2025.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga leo Aprili 9, 2025.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga leo Aprili 9, 2025.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya wazazi leo Aprili 9, 2025.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya wazazi leo Aprili 9, 2025.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya wazazi leo Aprili 9, 2025
Social Plugin