
Katika taarifa yake rasmi, Jambo Group of Companies imeeleza kuwa haihusiki na maombi yoyote yanayohitaji malipo kwa ajili ya ajira au mikataba. Kampuni hiyo imesisitiza kuwa mchakato wote wa maombi ya kazi, usaili na ajira hufanyika bila gharama yoyote kwa waombaji. Wananchi wamehimizwa kuwa makini na kutoridhia maombi yoyote ya malipo kwa ajili ya ajira, kwani ni ishara ya ulaghai.
Jambo Group of Companies imebainisha kuwa fursa halali za ajira na mikataba hutangazwa rasmi kupitia tovuti yake (www.jambogroup.co.tz) na ukurasa wake rasmi wa Instagram (@jambogroup). Wameonya kuwa mawasiliano yoyote kutoka kwa vyanzo visivyo rasmi yanapaswa kutiliwa shaka na kuthibitishwa kupitia njia zao za mawasiliano.
Wananchi wamehimizwa kuripoti mara moja matukio yoyote ya udanganyifu kwa vyombo vya usalama vya eneo lao au kuwasiliana moja kwa moja na kampuni kupitia info@jambogrouptz.net au +255 622 666 692.
Katika hatua ya kulinda umma dhidi ya vitendo vya kitapeli, Jambo Group of Companies imelaani vikali ulaghai huu na kusisitiza kuwa itaendelea kutoa ulinzi na mwongozo kwa wananchi. Wamewasihi watu wote kuwa waangalifu na kutumia njia rasmi za mawasiliano ili kupata taarifa sahihi na kuepuka kudanganywa.
Social Plugin