Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TASAC YAWAPIGA MSASA WADAU WA USAFIRI MAJINI MKOANI TANGA

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

Wadau wa usafiri wa maji wametakiwa kufuata masharti na taratibu za kazi zao na kuwa na weledi ili kuepuka kudhoofisha ufanisi na kuingia kwenye migogoro baina yao.

Wito huo imetolewa na Mkurugenzi Udhibiti Huduma za Usafiri Majini Nelson Mlali wakati wa mafunzo mafupi ya Sheria za majini iliyoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli nchini (TASAC).

Mlali amesema kumekuwa na tatizo la mgongano wa maslahi baina ya watoa huduma ambayo unawahusisha zaidi Mawakala wa Forodha dhidi ya Mawakala wa Meli lakini pia kuna tatizo la watoa huduma kutozingatia kanuni, masharti na taratibu zilizowekwa kuwaongoza.

"Pia kuna tatizo la ucheleweshwaji huduma zikiwemo mifumo, uwezo mdogo wa kiutendaji wa baadhi ya wadau, kutokana na matatizo haya tunajikuta tukiingia katika migogoro na gharama, hivyo kudhoofisha ufanisi na usafiri kwa njia ya maji " ,amesema.

Nitumie fursa hii kuwaomba, kufuatilia kwa umakini mjadala wa kikao hiki ili kwa pamoja tuweze kuboresha ufanisi, kupunguza migogoro na malalamiko katika sekta yetu ya usafiri kwa njia ya maji,

"Lakini pia naomba niwakumbushe kwamba, uwepo wa shehena, meli, bandari na maji pekee havitakuwa na tija kwetu iwapo hatutazingatia utii wa sheria na taratibu zilizowekwa kuongoza shuhuli zetu" ,amesisitiza.

Vilevile amesema mbali na hilo kuna utunzaji wa maji, ushiriki katika ulinzi na usalamanwa rasilimali zao na nchi kwa ujumla, pia ushirikiano katika kufanikisha taratibu mbalimbali zinaoongoza usafiri kwa njia ya maji.

"Uungaji mkono jitihada za serikali zinazolenga kuboresha mazingira ya usafiri kwa njia ya maji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kuboresha miundombinu ya usafiri wa ardhini,

"Ili kuziunganisha bandari zetu na masoko yake na jitahada za uboreshaji au ujenzi ili site kama Taifa tuweze kuneemeka na fursa zinazotokana na uchumi wa buluu" ,amesema.

Naye Ofisa Mfawidhi wa (TASAC) Mkoa wa Tanga Christopher Shalua amewataka wadau hao kuhakikisha wanazingatia afya na usalama kabla ya kutoa huduma za kupakua na kupakua mizigo kwenye Meli hususani zinazotoka nje.

Aidha Shalua aliwataka wadau hao kuhakikisha wanafuata Sheria na taratibu za nchi ikiwemo kuhusiaha lwseni zao ili waweze kupata ruhusa ya kufanya kazi zao bandarini wakati wote.

"Mawakala na wadau wote wanaotoa huduma za bandari lazima kuhakikisha kuwa vibali vyao vinahuishwa ili kufuata taratibu na Sheria za nchi yetu katika utoaji wa huduma bandarini", amesema Shalua.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com