Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JINSI WAANDISHI WATAKAVYOKWEPA HATARI ZA KIDIJITALI KATIKA WPFD 2025

 

Katika dunia ya sasa ambapo mashambulizi ya kimtandao na vitisho kwa waandishi wa habari vinaongezeka kila siku, maarifa ya kujilinda kimtandao si hiyari tena bali ni lazima.

Je, wewe kama mwandishi uko tayari kukabiliana na hatari hizi mpya?

Habari njema!
Kupitia maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani (WPFD) 2025, mashirika ya UTPC, MISA-TAN na OJADACT, kwa kushirikiana na UNESCO na JamiiForums, wameandaa kikao maalum cha mafunzo ya usalama na ulinzi kwa waandishi wa habari.

Tarehe: 28 Aprili 2025
Muda: 4:00 asubuhi – 3:30 jioni
Mahali: Ukumbi wa EAC, Arusha

Katika kikao hiki, utafundishwa:

  • Jinsi ya kufanya mawasiliano salama bila kuvuja kwa taarifa,

  • Mbinu za kuperuzi mtandaoni kwa usalama na kuficha utambulisho unapofanya uchunguzi wa habari,

  • Njia za kulinda data nyeti dhidi ya wavamizi wa kimtandao,

  • Namna ya kuripoti ukiukwaji wa haki zako kama mwandishi.

Kaulimbiu kuu mwaka huu ni:
"Reporting in the Brave New World: The Impact of Artificial Intelligence on Press Freedom and Media."

Katika zama hizi za akili bandia (AI), teknolojia imeleta fursa mpya lakini pia hatari mpya kwa wanahabari. Mafunzo haya yatakupa zana za kisasa za kujilinda na kulinda kazi zako.

Usikose! Hili ni tukio la kipekee kwa waandishi wanaotaka kusonga mbele kwa usalama na weledi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com