Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA NA SMAUJATA KWA MCHANGO WAKE KATIKA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa tuzo ya heshima na Idara ya Vijana, Hamasa na Mahusiano ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA), kwa kutambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kuimarisha ustawi wa Watanzania.

“Tunakutunuku tuzo ya heshima Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutambua na kuthamini mchango wako mkubwa katika maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii.”

Kwa mujibu wa uongozi wa SMAUJATA, Rais Samia amekuwa kielelezo cha uongozi wenye huruma, uwazi, na msukumo wa maendeleo jumuishi ,hususan kwa makundi maalum kama vile wanawake, vijana, watoto na watu wenye uhitaji maalum.

Mmoja wa viongozi wa idara hiyo amesema:
"Tuzo hii ni sauti ya vijana na jamii nzima ya Tanzania inayotambua ujasiri, hekima na moyo wako katika kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika safari ya maendeleo."


Tuzo hiyo ni ishara ya wazi ya heshima ya juu inayotolewa kwa uongozi unaoweka mbele ustawi wa jamii na maendeleo ya watu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com