Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga unatarajiwa kuzikwa Jumatano Aprili 16, 2025 wilayani Bunda mkoani Mara.
Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga ameyefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kuamkia Aprili 13, 2025 wilayani Bunda mkoani Mara, ambapo kwa sasa mwili wa Mhandisi Nyamo-Hanga umehifadhiwa katika Hospitali Teule ya DDH, Bunda.
Aidha, mwili wa dereva wake Muhajir Mohamed Haule ambaye alikuwa akiendesha gari hilo lililopata ajali unatarajiwa kusafirishwa muda wowote kuanzia sasa kuelekea Mlandizi wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya mazishi.
Social Plugin