Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI WAENDELEA NA UCHUNGUZI KIFO CHA MWANAFUNZI ALIYEJIRUSHA GHOROFANI ZANZIBAR

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linaendelea na uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha IT Madras mwenye asili ya Kihindi, aliyejirusha kutoka ghorofani huko Zanzibar.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, ACP Abubakar Khamis, amesema kuwa tukio hilo lililotokea Aprili 16, 2025, linaendelea kufuatilia kwa kina ili kubaini sababu zilizopelekea kijana huyo kuchukua hatua hiyo ya kujitoa uhai.

“Tunaendelea kufuatilia kwa undani ili kubaini kama kuna mazingira mengine yaliyomchanganya mwanafunzi huyo. Uchunguzi bado unaendelea,” amesema Kamanda Abubakar wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu chanzo cha tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com