
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza rasmi Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025, ambazo zitaleta mwelekeo mpya wa uchaguzi wa haki, huru, wa amani na unaoaminika kwa Watanzania wote.
Kanuni hizi zimeandaliwa chini ya Kifungu cha 162 cha Sheria ya Uchaguzi Na. 1 ya Mwaka 2024, kwa ushirikiano kati ya Tume, Serikali na vyama vyote vya siasa nchini.
🔍 LENGO LA KANUNI ZA MAADILI
Lengo kuu la Kanuni hizi ni kuhakikisha uchaguzi unazingatia:
👉Haki, uhuru na amani kwa wagombea na wapiga kura
👉Uwajibikaji wa vyama, Serikali, na Tume
👉Utulivu na uzingatiaji wa sheria na taratibu zote za uchaguzi
🧑🤝🧑 WAHUSIKA WA KANUNI
Wahusika wakuu ni:
👉Vyama vya siasa
👉Wagombea
👉Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
👉Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
Kila chama cha siasa na mgombea lazima wasaini na kuthibitisha kuheshimu Kanuni hizi kabla ya kushiriki uchaguzi.
🗣️ MAADILI KWA VYAMA NA WAGOMBEA
Vyama vya siasa na wagombea wanatakiwa:
👉Kuheshimu Katiba, sheria za uchaguzi na maelekezo ya Tume
👉Kufanya kampeni kwa amani, bila matusi, vitisho, au ubaguzi
👉Kutumia lugha ya Kiswahili au kutafsiriwa
👉Kusambaza mabango na vipeperushi vilivyoidhinishwa na Tume
👉Kutumia vyombo vya habari vya umma kwa usawa wa sera
Hairuhusiwi:
👉Kampeni katika nyumba za ibada
👉Kutoa rushwa, zawadi au hongo kwa wapiga kura
👉Kufanya kampeni usiku (baada ya saa 2:00 usiku)
👉Kuchochea vurugu au kutumia maneno ya chuki mitandaoni
👉Kubeba silaha au kuingilia mikutano ya vyama vingine
🗳️ MAADILI WAKATI WA UPIGAJI KURA
Katika siku ya kupiga kura:
👉Hairuhusiwi kuvaa sare za vyama au ishara yoyote ya kampeni
👉Wagombea na wafuasi wao wasifanye kampeni kituoni
👉Mawakala watasindikiza masanduku kwa kufuata utaratibu wa Tume
👉Malalamiko yawasilishwe kwa mujibu wa sheria
🏛️ MAADILI KWA SERIKALI
Serikali inapaswa:
👉Kutoa fursa sawa kwa vyama vyote
👉Kuweka mazingira ya usalama, hasa kwa makundi maalum (wazee, wanawake, watu wenye ulemavu)
👉Kutochanganya shughuli za Serikali na kampeni za kisiasa
Mawaziri na Wakuu wa Mikoa/Wilaya:
👉Hawaruhusiwi kutumia madaraka au rasilimali za Serikali kwa kampeni
👉Hawatakiwi kutoa ahadi mpya za maendeleo wakati wa kampeni
🏢 MAADILI KWA TUME HURU YA UCHAGUZI
Tume inatakiwa:
👉Kusimamia uchaguzi kwa haki, uadilifu na uwazi
👉Kutoa elimu ya mpiga kura kwa usawa
👉Kutoa ratiba za uchaguzi, kanuni na nyaraka kwa vyama kwa wakati
👉Kutotoa upendeleo kwa chama au mgombea yeyote
⚖️ USIMAMIZI WA MAADILI NA ADHABU
Kamati za Maadili zitatatua migogoro na malalamiko kwa ngazi zifuatazo:
👉Kata
👉Jimbo
👉Kitaifa
👉Kamati ya Rufaa
Adhabu kwa ukiukwaji wa Maadili ni pamoja na:
👉Onyo au karipio
👉Zuio la kufanya kampeni
👉Faini hadi Tsh 1,500,000/=
👉Tamko la umma la kuomba msamaha
👉Kifungo cha muda wa kampeni kwa wakiukaji wa ukatili wa kijinsia
✍️ TAMKO LA PAMOJA
Tume, Serikali na Viongozi wa Vyama vyote vya siasa wamesaini makubaliano ya pamoja kuthibitisha kuzingatia na kutekeleza Kanuni hizi kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2025.
Kwa taarifa zaidi tembelea:
🌐 www.inec.go.tz
🖋️ Habari hii imeandaliwa kwa kifupi na Malunde 1 Blog
BOFYA <HAPA> KUSOMA KANUNI ZA MAADILI YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI ZA MWAKA 2025
Social Plugin