Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC MASINDI AZUIA MAPENZI SHULENI ,ATUMA SALAMU KWA "WAKWEPA UMANDE"

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi

Na Sumai Salum -Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi amewataka wanafunzi kuwasaidia wazazi wao kazi pamoja  na kudumisha nidhamu kipindi hiki cha likizo.

Masindi ameyasema hayo Aprili 11,2025 alipokuwa na ziara ya kikazi Kata ya Talaga alipopita kuwasalimia wanafunzi wa Sekondari ya Talaga huku akiwahimiza elimu ndio chanzo cha mema yote katika maisha yao ya sasa na baadae.

"Msijihusishe na mapenzi na nyie ambao mnawapenzi acheni mara moja hao mabodaboda,wakulima,wajasiliamali,wafanyabiashara hawawezi kuwasaidia chochote pindi mtakapofeli mitihani yenu watawadanganya tu ili muwape penzi kisha wanawatupa kama chakula kilichoharibika",amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

"Mnapoenda likizo kawasaidieni kazi wazazi wenu,msitumike kivyovyote na wanasiasa kwelekea uchaguzi mkuu mwezi Novemba mwaka huu,epukeni makundi mabaya na kisha mjiimarishe kwa kuunda makundi hata ya watu sitasita ya kujisomea kumbukeni kuzaliwa masikini si shida Bali ukifa masikini ni ujinga wako", ameongeza Masindi.

Aidha amewahimiza wakati wa kuandaa hatima njema za maisha yao ya baadae ni sasa kwa kusoma kwa bidii na endapo akiwepo wa kufeli akumbuke maisha hayajaishia hapo kwani ziko elimu mbalimbali wanaweza kujiendeleza.

"Serikali yenu imetafuta fedha Tilion 1.3 ili kuwaletea maendeleo mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu mmeboreshewa madalasa,maabala,waalimu wa kutosha na vitu vingine vingi ili kila mtoto wa KiTanzania apate elimu bila kizuuzi sasa akikisheni mnarudisha fadhira kwa ufaulu wa hali ya juu.

Aidha ametuma salaamu kwa watoro na wanaopenda kudanganya ni wagonjwa ili wasihudhurie masomo amesema wanaharibu hatima zao na za familia zao na serikali haitosita kuwafuatilia na kuwachukulia sheria.

Amewakumbusha waalimu kufanya kazi kwa kufuata maadili na miiko ya kazi wakijitahidi kuongeza ufaulu na kutojihusisha kimapenzi na wanafunzi huku.

Masindi amewatakia sikukuu njema ya Pasaka wanafunzi na waalimu  huku akiwasihi washeherekee kwa kufuata dhumuni la sikukuu hiyo na kutovunja sheria za nchi.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu David Mashauri amesema halmashauri inajitahidi kutafuta fedha kupitia kwa wadau  mbalimbali na kutenga bajeti zake ili kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia.

"Tunao wadau mbalimbali wanajitahidi pale tunapohitaji uwezeshaji wao lakini pia niwapongeze wazazi wamekuwa na utayari wa kuanzisha vyumba vya madalasa,nyumba za walimu pamoja na matundu ya vyoo ila niendelee kuwahimiza kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni ili wasiwaze mengine zaidi ya masomo", amesema Mashauri












Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com