Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BABU AUA MJUKUU WA SIKU 2 KWA KUMBAMIZA CHINI, CHANZO BINTI KUZAA NA BABA MDOGO - SHINYANGA

NB- Picha haihusiani na habari


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Mtoto mchanga wa siku mbili mkazi wa Kijiji cha Shatimba, Kata ya Nyamalogo, Wilaya ya Shinyanga, anadaiwa kuuawa kikatili na babu yake aitwaye Maganga Lupalagula Mungo kufuatia mgogoro wa kifamilia.


Akizungumza na mwandishi wetu leo Aprili 11,2025 Mwenyekiti wa Kijiji cha Shatimba, Kalonga Shilu, amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa tatu usiku baada ya babu huyo kuomba kupwa mtoto ili amuone.

“Tulipokea taarifa kuwa Maganga Mungo alimchukua mjukuu wake kutoka kwa mama yake kisha akambamiza chini na kusema kuwa anamuua mtoto, mama na binti yake. Ni tukio la kusikitisha,” amesema Mwenyekiti Shilu.

Inaelezwa kuwa familia hiyo imekuwa na mgogoro wa muda mrefu baada ya binti wa familia kuolewa na baba yake mdogo na kuzaa naye mtoto huyo.

Hali hiyo imesababisha hasira kubwa kwa baba wa msichana huyo ambaye alichukua uamuzi huo wa kikatili.

Aidha, Mwenyekiti amesema kuwa baba huyo alikuwa ameombwa alee mtoto hadi afikishe umri wa miaka mitatu ambapo angekuja kulipwa gharama zote, jambo ambalo alilichukulia tofauti na kuamua kuchukua sheria mkononi.

Paul Maige, mkazi wa kijiji hicho, amesema kitendo hicho ni cha kinyama na hakiwezi kuvumilika katika jamii, akisisitiza umuhimu wa kushughulikia migogoro ya kifamilia kwa njia ya mazungumzo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,ACP Janeth Magomi, amesema hana taarifa kuhusu tukio hilo lakini ameahidi kulifuatilia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com