Na Barnabas kisengi Dodoma
Mbunge wa Jimbo la dodoma ambaye pia ni Waziri wa Madini Mhe Anthony Peter Mavunde amehudhulia uzinduzi wa Baraza la Wazee wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Jijini Dodoma
Mavunde amesema kuwa Wazee ni hazina kubwa hivyo wanapaswa kutunzwa na kuhakikisha mawazo na michango ya Wazee inachukuliwa na kufanyiwa kazi ili kuleta tija kwenye Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani
"Niseme bila kupepesa macho Mimi ni mzaliwa wa kata hii ya kilimani mtaa wa Nyerere hivyo leo nimefarijika sana kuwa miongoni mwa walioshuhudia uzinduzi mzuri mliofanya viongozi wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani kwa kuanzisha baraza hili la Wazee tukikumbuka huwa tunaambiwa Wazee ni hazina,
hata Mimi hapa niliko fika leo humu ndani naona Wazee wengi walionilea walimu wangu nawaona hivyo kwakuwa Mimi ni Mtoto wa kilimani hivyo Wazee nitatumika sana kwenu kwa jambo lolote mtakalo itaji msaada kutoka kwangu nimesikia risala yenu hivyo nitakaa na mwenyekiti wenu na viongozi wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani ili kuhakikisha yote mliyo yaeleza ninayatekeleza kama Mtoto wenu na Mbunge wenu ambaye ninatokea kata hii ya kilimani"amesema Mavunde
Aidha Mhe Mavunde amesema hivi karibuni anatarajia kutoa matofali elfu 40 na mifuko ya saruji 40 kwa kila kata katika kata zote 41 za jimbo la Dodoma hivyo amewataka Viongozi wa chama cha Mapinduzi kata zote kuhakikisha wanashirikiana na viongozi wa serikali kata na mitaa kuangalia wanaweza kufanya nini katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Mbunge mavunde pia amesema kwakuwa anakata 41 na mitaa zaidi ya 200 hivi karibuni anatarajia kugawa vishikwambi kwa wenyeviti wote wa Serikali za mitaa yote katika Jimbo lake.
Kupitia vishikwambi hivyo atakuwa ameunganisha mfumo wa tehama na ofisi yake ya Mbunge na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ili kuhakikisha utatuzi wa Changamoto au jambo lolote.
Social Plugin